Wakulima
wilayani hapa, ambao pia ni wafugaji wa
nyuki wamewataka wataalamu wa mifugo kuwatembelea vijijini kutoa elimu juu ya ufugaji nyuki kwa njia ya
kisasa.
Wakulima
hao walitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti
kwenye Maonesho ya Wakulima ngazi
ya vijiji yaliyofanyika juzi, Kata ya Diongioya, Tarafa ya Turiani wilayani
humo.
Wakulima kutoka vijiji 26 vya Tarafa ya Turiani na Mvomero walipata fursa ya kushiriki maonesho hayo maalumu yaliyoandaliwa na
Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata).
Hivyo
walisema, ufugaji wa nyuki hauna gharama kubwa na wanachokikosa ni kupata elimu
ya ufugaji wa kisasa utakaowaletea kipato chenye tija.
Wakulima
hao walisema, wanachokihitaji ni kupatiwa elimu ya ufugaji nyuki kwa njia ya
kisasa ambayo itawasaidia katika suala
la kutunza mazingira ya misitu ya asili.
Mkulima
na mfugaji wa nyuki wa Kijiji cha Hembeti, Bakari Shaaban, alisema kuwa licha
ya kuendesha kilimo cha mpunga katika bonde la Mkindo, pia ameamua kufuga nyuki
na kwamba mazao ya asali yamekuwa yakiwapatia kipato wakati huu ambao soko la
mpunga limedorora.
Hata
hivyo alisema, kufuatia wakulima wengi katika kijiji na kata hiyo ya Hembeti
kujitokeza kufuga nyuki, mahitaji yao makubwa ni kupatiwa utaalamu wa ufugaji
wa kisasa na kupata aina bora ya mizinga ya kufugia nyuki.
Kwa
upande wao, wakulima wa Kijiji cha Dihinda, katika Kata ya Hembeti, Amina Ally
pamoja na Omary Athuman kwa nyakati tofauti walisema, ukosefu wa soko la mazao
kumetoa mwanya kwa walanguzi kuwalalia kwa kununua mazao yao kwa bei ndogo.
No comments:
Post a Comment