Watu
wasiojulikana wilayani Manyoni wamemchinja mithili ya kuku binti mmoja anayekadiriwa
kuwa na umri wa miaka 16.
Diwani wa
Kata ya Manyoni Mjini, Hamis Masabuni alisema tukio hilo lilitokea juzi asubuhi
katika eneo la Mitoo kwenye mashamba ya Magereza, Uwanja wa Ndege wa zamani.
Alisema siku
ya tukio, yeye alipata taarifa ya simu kutoka kwa raia wema hivyo ikambidi
aende huko kushuhudia kulikoni na mara
alipofika eneo hilo alikuta mwili wa
marehemu ukiwa umelala chini na kuchinjwa mithili ya kuku.
Diwani huyo
amelitaka jeshi la polisi kufanya
uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo ili kubaini wauaji wa binti huyo ili hatua
za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Muuguzi wa
zamu katika hospitali ya wilaya ya Manyoni, Getruda Njughuda amekiri kuupokea mwili wa binti huyo.
Naye Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alisema kuwa polisi inaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo.

No comments:
Post a Comment