Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias
Chikawe amesema si vema kuhusisha
masuala ya milipuko ya mabomu katika mikoa mbalimbali kuwa ni ugaidi bali kila
tukio kuchukuliwa kwa pekee.
Aidha, alikanusha kuwa matukio hayo yanahusika na utalii, kwani yangepigwa mikoa ya Kilimanjaro na Dar es Salaam ambapo kuna utalii mkubwa zaidi.
Akizungumzia milipuko iliyojitokeza hivi karibuni wakati akihojiwa na kituo cha redio cha Clouds jijini Dar es Salaam, Chikawe alisema hali ya usalama nchini ni nzuri na iko imara na vitendo hivyo ni vya kihalifu na wizara inashughulikia ipasavyo.
Alizungumzia tukio la mara ya mwisho lililohusisha wafanyabiashara na inawezekana ikahusisha masuala hayo ya kibiashara kutokana na kushambulia wafanyabiashara.
Alisema kila hatua ya upelelezi ikikamilika watatoa maelezo kwa wananchi na sasa wanaendelea vizuri na kuamini kuwa watafanikiwa kuwapata wahalifu.
Alipoulizwa ni kwa nini milipuko hiyo inatokea Zanzibar na Arusha pekee na kuhusiana na masuala ya utalii, Chikawe alikanusha kuwapo kwa uhusiano wa utalii na mabomu hayo kwani anaamini hata Dar es Salaam na Kilimanjaro nayo ni maeneo ya kitalii zaidi.
“Ni lazima tuamini na kufanya matukio haya ni ya wahalifu na tuyashughulikie hivyo na siyo kuingiza mambo mengine kwani tutafanikiwa tu kwa kutumia taaluma zetu za kipolisi,” alisema.
Alisema baada ya uchunguzi watajua kwa nini yametokea na kutoa taarifa kwa wananchi ni lazima sasa kusubiri kwani hata polisi kutokana na sababu hiyo watakuwa wamejifunza.
Chikawe aliwataka watalii kuendelea kuja nchini kwani wanawahakikishia usalama wao na mali zao na hakuna matatizo yoyote na vitendo vinavyotokea ni vya kihalifu na vitashughulikiwa kama vingine nchi nzima.
Akizungumzia malalamiko ya watu kuchelewa kuwakamata wahalifu, alisema wanafanya hivyo ili kuwa na uhakika wa watuhumiwa na siyo kuzoa watu na baadaye kushindwa kesi kutokana na kukosa ushahidi.
Chikawe alisema kushindwa kwa kesi za aina hiyo kunakatisha tamaa wananchi, hivyo polisi wapewe muda ili kuhakikisha wanawapata watuhumiwa hao.
Akizungumzia matukio hayo kujirudia mara kwa mara, alisema ni suala la wahalifu na ili kukabiliana nayo ni vema wananchi kurudia tabia za zamani za wanapoona wageni ambao hawaeleweki wakatoe taarifa.
“Ni vema kurudi katika utamaduni wetu wa awali kwa kuacha masuala la utandawazi kwa kutambuana na yeyote mgeni ni vema kumfuatilia na kutoa taarifa ikiwa hawana taarifa zake," alisema.
Alisema wageni kutoka nchi nyingine wanaweza kuingia nchini na kufanya vitendo vya hatari hivyo ni vema ulinzi wa nchi kuanzia kwa wananchi kwa kutoa taarifa mapema na hatua kuchukuliwa.
Chikawe alizungumzia suala la kutokuwepo kwa usiri baina ya wananchi wanaotoa taarifa polisi kuwa ni sababu ya wananchi kuogopa kufanya hivyo kwani askari polisi wanapeleka taarifa kwa wahalifu.
Alisema jeshi la polisi lina watu makini walioelimika na kufuata sheria hivyo iwapo suala hilo litatokea atatoa namba zake za simu ili wananchi wamtaarifu na yeye kuchukua hatua stahili kwa Polisi hao wasio na siri.
Kauli hiyo ya Chikawe imekuja siku moja baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu kusema jeshi hilo lina uhakika wa kuwapata watuhumiwa wa mabomu mkoani Arusha na kwingineko nchini, pamoja na kudhibiti matukio hayo baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa taarifa walizopata.
Tangu mwaka huu kuanza kumetokea zaidi ya matukio matatu ya bomu mkoani Arusha, yakiwemo ya Aprili ambapo watu kadhaa walijeruhiwa na mmoja Sudi Ramadhan alipoteza maisha baada ya bomu kurushwa kwenye baa ya Night Park iliyopo Mianzini.
Pia katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan, Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini wa Taasisi ya Kiislamu ya Answar Muslim Youth Centre, Shehe Soud Ally Soud alijeruhiwa kwa bomu akiwa na mgeni wake kutoka Kenya, Shehe Muhaji Hussein Kifea wakati wakila daku nyumbani kwake eneo la Majengo. Kifea amevunjwa miguu yote miwili na kupoteza vidole vitatu vya mguu wa kulia.
Pia watu wengine wanne wenye asili ya Asia wamejeruhiwa kwa bomu akiwemo mmoja aliyepoteza mguu wakati bomu lilipovurumushwa kwenye mgahawa wa Vama Traditional Indian Cuisine.

No comments:
Post a Comment