Jeshi la polisi mkoani Ruvuma linawatafuta
wakazi wawili wa kijiji cha Silo kata ya Linda wilaya ya Nyasa kwa tuhuma za
kumbaka msichana wa miaka 10 , mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya Msingi
Luhekitiki wilayani humo.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Mihayo Msikela alimtaja mtuhumiwa wa kwanza kwa jina moja la Damas ambaye kwa kushirikiana na mwenzake ambaye hakufahamika walimbaka mwanafunzi huyo nyakati za usiku katika kijiji hicho.
Tukio hilo lilitokea juzi usiku ambapo Damas akiwa na mwenzake, walimrubuni mtoto huyo kwa pipi na kumvuta kichakani kabla ya kumbaka.

Alisema mwanafunzi huyo alikuwa katika sherehe za ngoma kijijini hapo.
Alieleza kuwa watuhumiwa hao
baada ya kufanikisha lengo lao hilo
walikimbia na kumuacha mtoto huyo kichakani akipiga kelele kabla ya kuchukuliwa na
wasamaria ambao walitoa taarifa kwa babu yake (jina limehifadhiwa) ambaye naye
alitoa taarifa ya tukio hilo polisi.Baada ya polisi kufika kijiji hapo na kumchukua mtoto huyo walimfikisha
hospitalini kwa ajili ya uchunguzi na aligundulika kufanyiwa kitendo hicho.

No comments:
Post a Comment