Wajawazito
1,031 wamegundulika kuwa na virusi vya Ukimwi kwa kipindi cha kuanzia Januari
hadi Desemba mwaka jana.
Hayo
yalisemwa juzi na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Ezekiel Mpuya wakati wa uzinduzi wa kampeni
ya kutokomeza virusi ya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Dk
Mpuya alisema katika kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka jana, Mkoa uliwapima wajawazito 66,555, ambapo kati
yao 1,031 waligundulika na virusi vya Ukimwi ikiwa ni sawa na asilimia 1.5.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Neema
Rusibamaila alisema Ukimwi unasababisha asilimia sita ya vifo vya watoto walio
chini ya miaka mitano.
Hata
hivyo Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Tunajali, Dk Joseph Mweshemi alisema lengo la
mradi huo ni kutokomeza maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda
kwa mtoto.
Alisema
mradi huo ulioanza mwaka 2007 umefanikiwa kutekeleza mambo mengi ikiwemo
kupunguza maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Watoto wengi
walioathirika na VVU ni wale waliopatikana kutokana na mimba zisizotarajiwa.

No comments:
Post a Comment