Mkazi
wa Kijiji cha Nyamuswa, wilayani Bunda Mkoa wa Mara, Sumera Sungura (28), anashikiliwa na Polisi
akituhumiwa kutaka kunyonga mtoto wake wa kufikia kwa kumning’iniza kwenye mti
wa mwembe.
Polisi
imetaja mtoto aliyetaka kuuawa ni Adamu Adamu (5). Kwa mjibu wa Mwenyekiti wa
Dawati la Jinsia wa Kituo Kikuu cha Polisi Wilaya ya Bunda, Ritha Charles,
tukio hilo ni la Juni 6, mwaka huu kijijini hapo.
Inadaiwa
baba huyo alitaka kufanya kitendo hicho
wakati mama wa mtoto huyo, Nyabakira Adamu alipokuwa amelazwa
hospitalini.
Ofisa
huyo wa Polisi alidai, baba huyo alikamatwa juzi na kwamba leo atafikishwa
mahakamani, kujibu tuhuma ya kukusudia kuua mtoto huyo.
Taarifa zinadai mtoto huyo ambaye mama yake alimzaa kabla
kuolewa na mtuhumiwa huyo, alinusurika kifo baada ya mchungaji wa ng’ombe wa
mtuhumiwa, kumkuta akining’inia kwenye mwembe povu likimtoka mdomoni.
Alimnusuru kwa kukata kamba.
Akizungumza
kwa tabu na mwandishi wa habari hizi, mtoto huyo alisema siku ya tukio baba
yake huyo alimkuta barabarani na kumkamata na akaanza kumpiga akihoji sababu za
kucheza barabarani.
Alieleza
kwamba, baada ya kupigwa alifungwa kamba shingoni na kuning’inizwa mtini, na
kisha baba yake alitokomea.
“Hakunipeleka
hospitali, alikuwa ananipaka dawa ya ng’ombe hapa (anaonesha alama za majeraha)
akinitishia kunipiga tena nikisema kwa watu,” alisema mtoto huyo.
Aidha, ilielezwa kuwa baada ya tukio hilo mama
mzazi wa mtuhumiwa huyo alipotaka kumchukua, ili akatoe taarifa Polisi juu ya
unyama huo, mtuhumiwa alimtishia na ndipo
alipotoa taarifa kwa mama yake mdogo amfuate.
Bibi
wa mtoto huyo, Nyanzara Mwikwabe , alisema alipata taarifa kutoka kwa majirani,
na baada ya kumuona ana michubuko shingoni alimchukua na kumpeleka nyumbani
kwake na kisha akatoa taarifa Polisi.
Ofisa
Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Bunda, Beatrice Gwamagobe, alikiri kuwepo tukio
hilo na kuongeza kuwa mtoto huyo juzi alifikishwa ofisini kwao na Mwenyeti wa
Dawati la Jinsia kutoka Polisi Bunda.

No comments:
Post a Comment