Friday, April 11, 2014

SUMAYE KUUNGURUMA KESHO CHUO KIKUU CHA HAVARD

Aliyekuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye kesho anatarajiwa kuunguruma kwenye Kongamano la 20 la Kimataifa la Chuo Kikuu cha Harvard huko Boston nchini Marekani.

Taarifa kutoka mjini hapa zimeeleza kuwa kongamano hilo la Kimataifa litakutanisha wasomi, wanasiasa na watu mashuhuri  zaidi ya 400 kutoka sehemu mbalimbali duniani likiwa chini ya mada isemayo; “Ni wapi duniani tulikosea katika masuala ya maendeleo?
Miongoni mwa wanasiasa watakaohudhuria kongamano hilo kutoka Ukanda wa Afrika  Mashariki pamoja na Sumaye, ni aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga.
Harvard ni moja ya vyuo vikuu vinavyoheshimika zaidi duniani ambapo Sumaye ni mmoja wa wanafunzi waliosoma chuoni hapo na kesho anatarajiwa kuwa mzungumzaji katika mada hiyo kwa kuoanisha maudhui ya mada hiyo na uzoefu wake kwa Bara la Afrika.

No comments: