Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), tawi la jijini Washington DC, Marekani wametoa tamko la kuunga mkono muundo wa serikali mbili, wakisema umewaweka Watanzania katika hali ya umoja na mshikamano kwa miaka ipatayo 50 sasa.
Tamko hilo limetolewa jijini Washington DC, Marekani juzi na uongozi wa tawi hilo chini ya Mwenyekiti wake, George Sebo walipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
“Sisi tunaunga mkono serikali mbili kwa sababu ya kazi nzuri iliyoifanya na bado inaendelea kufanya ya kuwaweka watanzania katika hali ya umoja na mshikamano," alisisitiza Sebo.
Alitahadharisha kwamba serikali zikiwa tatu zitahatarisha umoja wa watanzania.
Kwa mujibu wa Sebo, tawi la CCM Washington DC lina idadi ya wanachama 330 kutoka maeneo matatu ya Virginia, California na Maryland huku wakiendelea kusaka wanachama zaidi kutoka maeneo mengine nchini Marekani.
Kuhusu hoja ya uraia wa nchi mbili ambalo pia linaendelea kujadiliwa kwa kasi yake kwa siku za hivi karibuni, Sebo ametoa ombi maalumu kwa serikali na CCM kuchukua hatua za makusudi za kuwaelimishwa kwanza wananchi faida na hasara ya kuwa na utaratibu huo kabla ya kufanyika kwa maamuzi ya kukubalika au kukataliwa.
Wakati huo huo, wazee wa Baraza la Chama Cha Mapinduzi Zanzibar wamempongeza na kumshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa ufafanuzi na kuunga mkono hotuba yake kwa Bunge la Katiba aliyoitoa tarehe 21 Machi, Mjini Dodoma.
Wazee hao wametoa tamko lao Ikulu juzi.
“Wazee wote tunakushukuru, tumefurahishwa sana na Hotuba ile kwani umetoa ufafanuzi wa mambo mengi, kwa hivyo tumefika hapa kukufahamisha kuwa tumefurahishwa sana, tuko pamoja nawe kwa hali ya aina yoyote" wamesema na kumueleza Rais kuwa wanayo mabaraza katika Wilaya, Mikoa, Kata na hata Mashina.
“Tumefurahi sana, hotuba hii imetufungua na tumefunguka hivyo tunakuunga mkono na tuko nawe katika hoja ya Serikali mbili kama ilivyo katika Chama Chetu.” Wazee hao waliongozwa na Khadija Jabir Mohammed ambaye ndiye kiongozi wao na Waziri Mbwana Ali Katibu wa Wazee.
Wazee wengine waliofika Ikulu ni Juma Ame Juma, Mohammed Khamis Haji, Juma Khamis Khamis na Tabib Omar Makungu. Wengine ni Alchui Khamis Alchui, Abdallah Rashid Abdalla na Haji Machano Haji.
Rais Kikwete aliwashukuru Wazee hao kwa kumtia moyo kwa kufika Ikulu kuelezea hisia zao ambapo Rais amewaeleza Wazee hao kuwa takwimu zote alizotumia katika Hotuba yake amezitoa kwenye ripoti ya Tume ya Jaji Warioba na kwamba hata maswali aliyokuwa akiuliza, alikuwa akiyauliza kwa nia ya kuyatafutia majibu na majawabu ya misingi kama yalivyoandikwa kwenye rasimu ya Tume
“Takwimu zote nimetoa kwenye taarifa ya Tume, maswali niliyouliza nimeyatoa kwenye taarifa, pia kuna mambo ya uandishi ambayo hayakuwa yameandikwa sawasawa hivyo nina wajibu wa kutoa tahadhari kwa wajumbe wa tume ili kuwa na uhakika wa dhana na tafsiri zilizomo kwenye rasimu ya Tume,” Rais Kikwete amefafanua zaidi.

No comments:
Post a Comment