Halmashauri ya wilaya ya Bahi kwa kushirikiana na hospitali ya Dodoma Medical Christian Medical Clinic(DCMC ) na Shirika la Maendeleo la Uswisi, wanatarajiwa kufanya kampeni kubwa ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi wilayani Bahi.
Uchunguzi huo utafanywa kwa akina mama wa tarafa mbili za Bahi na Chipanga ili kuwabaini walio pia katika hatari ya kupata ugonjwa huo.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi inayotarajiwa kufanyika katika Halmashauri ya wilaya ya Bahi Aprili 14 mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Alisema Aprili 13, kutakuwa na zoezi la kujiandikisha na matarajio ni kuwafikia zaidi ya akina mama 1,600 na watakaogundulika na dalili za awali za ugonjwa huu, watapatiwa matibabu bure.
Aliwataka wanawake na wasichana kujitokeza na kuachana na imani potofu za akina baba wanaovumisha kuwa wanawake wanakwenda kutolewa mayai ya uzazi.
Wanawake zaidi ya 250,000 hupoteza maisha kila mwaka duniani kutokana na kuugua ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.
Aidha Shirika la Afya Duniani (WHO), linakadiria kuwa kila mwaka wagonjwa wapya 500,000 wa saratani ya shingo ya kizazi hugundulika na kati ya hao zaidi ya 250,000 hufariki dunia kutokana na kukutwa hatua za mwisho za ugonjwa huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa wilaya hiyo Rachel Chuwa amewataka wananchi hususan akina mama kujitokeza kwa wingi kupata huduma mbalimbali zitakazotolewa katika zoezi hilo huku akiwataka akina baba kuwaruhusu akina mama kwenda kupatiwa uchunguzi na matibabu.

No comments:
Post a Comment