KANISA LAENDESHA BAHATI NASIBU YA BUNDUKI ILI KUVUTIA WATU WENGI...

KUSHOTO: Tangazo la bahati nasibu. KULIA: Kanisa la Grace Baptist.
Kanisa moja lililoko mjini New York limejinadi kutoa bure bunduki aina ya AR-15 kwenye bahati nasibu itakayofanyika baadaye mwezi huu, kama sehemu ya jaribio la kuvutia watu wengi zaidi kwenye Kanisa la Grace Baptist huko Troy limekuwa likisambaza vipeperushi vinavyosema "Shinda AR-15 ya BURE" sambamba na nukuu kutoka Agano Jipya la Biblia inayosomeka: "...amani yangu nawapeni ... Yohana 14:27."

Mchungaji John Koletas ametetea utoaji huo wa bunduki, akisema ni tukio la kuwapa heshima wawindaji na wamiliki wa bunduki katika eneo hilo, imeripotiwa.
"Biblia imeshiba katika kujichunga mwenyewe na kujilinda mwenyewe, na kuweza kujichunga mwenyewe," Mchungaji John Koletas alisema.
"Tunawaheshimu wamiliki wa bunduki na wawindaji.
"Na tumekuwa baraka na msaada kwa watu ambao wamekuwa wakishambuliwa, wakishambuliwa vikali, na wanajamii wenye hasira kali na watu wanaopinga Ukristo - wanasiasa na vyombo vya habari.
Kipeperushi hicho cha promosheni kinasema: "Je, Biblia inalinda haki zangu kuhifadhi na mikono halisi? Mhudhuriaji aliyefuzu atapata bunduki aina ya AR-15 iliyokarabatiwa kisheria ...Zawadi zote hizo kiingilio ni bure kabisa.
"Nchi yetu iliundwa na Mfalme James Bible na bunduki."
Bunduki hiyo aina ya rifle iliyoundwa na Smith & Wesson M&P, toleo la mtengenezaji la AR-15, imetolewa na duka moja la mjini humo na kutimiza vigezo vyote vya masharti ya udhibiti yaliyomo kwenye sheria inayofahamika kama Sheria ya USALAMA.
Tukio hilo litafanyika Machi 23, mwaka huu.
Mbunge Steve McLaughlin, ambaye anawakilisha taasisi hiyo na ambaye atazungumza kwenye shughuli hiyo, alisema anafikiri bahati nasibu hiyo ni ya kawaida kabisa.
"Ni bidhaa iliyopo kisheria. Makanisa huuza kwa bahati nasibu bidhaa mbalimbali wakati wote," alisema.
"Kanisa langu hufanya bahati nasibu ya Dola za Marekani 10,000 kila mwaka. Namaanisha, sifahamu kwanini kumekuwapo na utata, kwa hakika, ni imefungwa kisheria wananchi waendao kanisani wa New York ambao ni wamiliki wa bunduki kisheria wanashiriki kwenye bahati nasibu kuchangisha fedha kwa ajili ya kanisa fulani. Sielewi utata huo unatokea wapi."
Ajabu, kanisa hilo liko mwendo wa masaa mawili kwa gari kutoka Shule ya Awali ya Sandy Hook huko Newtown, Conn, ambako wanafunzi 20 wa darasa la kwanza na wafanyakazi sita walipigwa risasi Desemba, 2012.
Baadaye mtu huyo mwenye silaha, mwenye miaka 20 Adam Lanza, akajipiga risasi mwenyewe.
Wakati bahati nasibu ya bunduki inaweza kuwa jambo geni katika eneo hilo, ni jambo la kawaida matukio kama hayo makanisani kwingineko nchini humo, kama Kentucky.
Kwa mujibu wa gazeti la The Los Angeles Times, Kanisa la Lone Oak First Baptist lilivuta watu takribani 1,300 ndani ya bwalo lao kwa kutoa bunduki 25 kwa wakati mmoja.
Mpenzi wa bunduki, Chick McAlister, pia alisimulia kuhusu bunduki na dhambi na Yesu.
"Hakuna serikali katika uso wa dunia hii ambayo ina haki ya kuninyang'anya bunduki," McAlister aliuelezea umati uliofurika ukumbini humo.

No comments: