Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi nyaraka Dk Thomas Kashililah mara baada ya kumwapisha jana. |
Katibu huyo jana aliapishwa na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo huku akiahidi kufanya kazi yake kwa weledi mkubwa na kwa kufuata kanuni za Bunge hilo.
Akizungumza baada ya kuapishwa, Hamad ambaye atasaidiwa na Katibu msaidizi Dk Thomas Kashililah, alisema hatakuwa na upendeleo wowote wakati wa kutekeleza majukumu yake ya ukatibu wa Bunge hilo la kihistoria.
Aliahidi pia kuwa hataweza kuchanganya mambo yake binafsi kutenda kinyume cha kanuni zinavyoelekeza na akaeleza kuwa majukumu hayo ni mazito ambayo yanahitaji awe mwaminifu na mkweli zaidi.
Alisema atatumia uzoefu wake wa ukatibu wa baraza la wawakilishi kuhakikisha kuwa kila mjumbe wa Bunge hilo anapata nafasi ya kuchangia kuhakikisha rasimu ya pili ya katiba inakuwa na mchango wa kila mjumbe aliyeko ndani ya Bunge hilo.
Pia alisema kwamba yeye na timu yake ya utendaji wa kila siku watahakikisha wanaandaa vikao ambavyo vitakuwa na tija ambavyo vitawaelekeza wajumbe wanachangia kuweka utanzania mbele katika mijadala ambayo watakuwa wanaifanya.
Hamad alisema anatumaini ataifanya vizuri kazi yake kwa tayari wana kanuni ambazo zitafuatwa wakati wote wa uendeshaji.
Alisisitiza kuwa ni lazima kuwe na utashi wa kisiasa katika kupitisha ibara za rasimu ya katiba kwa vile Watanzania wanatarajia kupata katiba ambayo itaweka mazingira mazuri katika shughuli zao za kila siku.
Kwa upande wake Dk Kashililah alisisitiza kufuata kanuni za Bunge hilo katika kuwatumikia wabunge wote.Sherehe hizo za kuwaapisha makatibu hao wa Bunge maalumu zilihudhuriwa pia na viongozi kadhaa ambao ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Seif Ali Idd, na wengineo.
No comments:
Post a Comment