Baadhi ya abiria wakikabiliana na kero ya usafiri Stendi Kuu ya Mabasi ya Mikoani Ubungo. |
Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), imetangaza namba za simu zinazoweza kutumiwa na abiria kuripoti kero na uvunjwaji wa sheria za barabarani, unaofanywa na madereva na makondakta wa daladala wawapo safarini.
Aidha, pamoja na kuripoti maovu ya wahusika hao wa daladala, Sumatra imetaka wanaotumia usafiri huo, hususan Dar es Salaam, kushirikiana kukamata na kuwafikisha Polisi madereva na makondakta husika, hatua zaidi za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Ofisa Mfawidhi wa Sumatra, Conrad Shio alitaja namba hizo ni 0755660016 na 0754864829 ambazo zinaweza kutumiwa na abiria wakati wowote kuanzia asubuhi hadi saa 5:00 usiku.
Katika hatua nyingine, Shio alisema abiria wanaruhusiwa kukamata na kuwafikisha polisi madereva na makondakta wa daladala wanaovunja sheria za barabarani, bila kujali umri wao wala uwezo na nguvu za wamiliki.
Alisema ushirikiano wa abiria katika kuripoti kero, kutoa ushahidi, kukamata wahusika na kuwafikisha panapohusika, ndiyo njia ya awali inayoweza kuzuia wasiendelee kutendewa ndivyo sivyo wawapo safarini.

1 comment:
Namba inayoanza na 08 ndo yenyewe na sio hizi
Post a Comment