KANISA KATOLIKI LAWATOA HOFU WAUMINI WAKE KUHUSU SAKRAMENTI...

Uongozi wa Kanisa Katoliki nchini umewatoa hofu waumini wake, kuhusu uwepo wa baadhi ya makanisa yanayodaiwa kuuza sakramenti na kueleza kuwa suala hilo haliwahusu. Katibu Mtendaji wa Idara ya Mawasiliano ya Jamii wa TEC, Padri Anatory Salawa aliliambia gazeti hili jana kuwa, matumizi ya sakramenti ni mapokeo ya Kanisa Katoliki na yanaporipotiwa isivyo ni sawa na kupotosha imani, ambayo msingi wake ni Yesu Kristo.
“Sakramenti ndio ukweli wa Neno la Mungu wenyewe kwa imani ya Kanisa Katoliki, na zipo saba; Ubatizo, Kipaimara, Ekaristi Takatifu, Kitubio, Mpako Mtakatifu, Ndoa na Daraja Takatifu ambalo ni Upadri, ikitokea imani hii ikatumika vibaya, inawapotosha waumini,” alifafanua Padri Salawa.
Mwandishi alinukuu baadhi ya waumini  wa Kanisa la Break Through Assemblies la Mchungaji Godfrey Simtomvu, wakilalamikia kuuziwa chakula cha bwana kwa Sh 100,000 katika ibada. Chakula hicho kilitajwa kuwa ni Sakramenti, neno linalotumiwa zaidi na makanisa ya Katoliki, Anglikana na Walutheri.

No comments: