Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mtanda akiingia shuleni. |
Mganga mfawidhi katika kituo cha afya mjini hapa, Dk Enock Chilumba ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi.
Alisema ametoa huduma kwa wanafunzi hao waliopelekwa kwenye kituo hicho kwa nyakati tofauti kuanzia saa 3.30 asubuhi hadi mchana.
Alisema kati ya wanafunzi hao 14 kutoka katika shule ya msingi ya Mtanda, wasichana ni 12 na wawili ni wavulana.
Alisema ugonjwa huo huwakumba watoto wa kike na mara chache kuwakumba wavulana. Hupata wenye umri wa miaka 10 na kuendelea. Maambukizi hayo yanatokana na wanafunzi wakiwa kikundi au wanacheza pamoja.
Aliwataja wanafunzi hao wa darasa la sita waliokumbwa na ugonjwa huo ni Hanifa Ngongi, Sharifa Mshamu, Dhulfa Isaa, Neema Sylivester na Six Mrope.
Wengine waliokumbwa na ugonjwa huo kutoka darasa la saba ni Fatuma Jumanne na Rehema aliyefahamika kwa jina moja. Wanaosoma darasa la tano ni Margreth Anthony, Zainabu Suma, Rehema, Hadija Hashimu na Variety Mwaisaka.
Hata hivyo alisema kuwa hali zao zinaendelea vizuri na wengine walitegemewa kutolea hospitalini jana.
Naye Ofisa elimu wa shule za msingi katika manispaa ya Lindi, Catherine Kihaule alithibitisha kuwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Mtanda wapatao 14 wako wodini katika kituo cha afya mjini hapa.
No comments:
Post a Comment