Mama Maria Nyerere. |
Siku moja baada ya kuripotiwa taarifa za uporaji wa kiwanja cha familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Serikali imeingilia kati na kuzuia ujenzi katika kiwanja hicho, uliokuwa ukiendelea kwa mabavu.
Mtoa taarifa wetu kutoka katika familia hiyo, alisema kuwa kibali kingine cha kuzuia ujenzi huo kimetoka jana saa tano asubuhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, kwenda kwa Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Oysterbay.
"Tumefarijika sana, kimekuja kibali leo hii (jana) saa tano asubuhi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya kwenda wa Mkuu wa Polisi Oysterbay kuzuia ujenzi uliokuwa ukiendelea," alisema mwanafamilia huyo.
Alisema kuwa hata vitisho walivyokuwa wakipata awali kutoka kwa watu hao, kwa sasa havipo.
Kwa mujibu wa mwanafamilia huyo, awali walipewa taarifa kuwa kikao cha pamoja kwa pande zote kingekaa jana, lakini baadaye wakaambiwa Rugimbana amepata dharura anaenda kusoma mafunzo ya wiki moja, haikufafanuliwa wapi.
"Kikao kilikuwa leo (jana), lakini tumeambiwa Mkuu wa Wilaya amepata udhuru anaenda kwenye kozi ya wiki moja, amemuachia DAS (Ofisa Tawala wa Wilaya) aendelee na kikao hicho, lakini bado hakuna taarifa tena rasmi," alisema.
Hata hivyo, mwandishi alimtafuta Rugimbana jana asubuhi baada ya kuahidi kutoa ufafanuzi zaidi, na alipopigiwa simu alisema angetoa taarifa mchana.
Mchana ulipofika saa nane, mwandishi aliwasiliana tena na Mkuu huyo wa Wilaya, akasema atapiga simu yeye mwenyewe ingawa mpaka tunaenda mitamboni, hakupiga simu.
Familia hiyo ya Baba wa Taifa, iliporwa kiwanja ilichokuwa inamiliki na mporaji mwenyewe alianza ujenzi chini ya usimamizi wa walinzi wa miraba minne.
Kiwanja kilichoporwa kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu, kiko Msasani Beach karibu na makazi ya mjane wa Mwalimu, Mama Maria na ni namba 778.
Mtoa habari huyo alibainisha kuwa waporaji hao walionesha kiburi kiasi cha kukaidi agizo la Polisi la kwanza lililowataka waache kuendelea na ujenzi katika eneo hilo mpaka litakapopatiwa ufumbuzi.
Kutokana na taarifa hizo, mwandishi alitembelea nyumbani kwa Mwalimu kuthibitisha taarifa hizo na kukutana na mwanafamilia mwingine, ambaye ni mkwe wa Mwalimu.
Mkwe huyo wa Mwalimu alimtaja mmoja wa wavamizi hao (jina limehifadhiwa) na amekuwa akidai kuuziwa kiwanja hicho na mtoto wa Mwalimu.
"Huyo mtoto wanayesema amewauzia hicho kiwanja anaumwa, hata kisheria haruhusiwi kuingia mkataba kwa hiyo tunarudi pale pale kuwa ni matapeli tu hawana jingine lolote," alisema.
Baada ya kuvamia kiwanja hicho, mtoa habari alisema waporaji hao wamefanya ujanja na kukigawa viwili; kimoja kina namba 778 na kingine 782, wakati awali kilikuwa na namba moja 778.
Alidai hata nyaraka wanazodai kuuziana na mtoto huyo wa Mwalimu zimeghushiwa, kwa kuwa mtoto mwenyewe alipoulizwa, alikana kuuza kiwanja hicho na kuongeza kuwa hata saini inayoonekana katika nyaraka hizo si yake.
Katika kuonesha kiburi cha waporaji wanaodaiwa kuwa wafanyabiashara, mtoa habari huyo alisema wamekuwa wakitamba kuwa hakuna mtu wa kuwafanya chochote huku wakihoji Mwalimu ni nani?
"Wanatamba hakuna mtu anayeweza kufanya chochote...wanafikia hatua ya kuhoji Nyerere ni nani, eti alikuwa zamani, lakini kwa sasa hana chochote. Hizi kashfa zinatukera," alisema.
Alisema pamoja na kukerwa na hali hiyo, wameamua kuacha suala hilo kwa vyombo husika, ili vichukue hatua na wamemteua wakili awasaidie.
"Sisi tunashindwa kuelewa, kwa sababu anafanya vile anavyotaka. Kuna kipindi alianza kumwaga kifusi, tukaenda kwa OCD (Mkuu wa Polisi wa Wilaya), akaja akamwambia aache kuendelea kumwaga kifusi,” alisema.
Alisema pamoja na agizo hilo la OCD, mfanyabiashara huyo ameendelea kumwaga kifusi katika eneo hilo ili kuanza ujenzi na shughuli hiyo hufanyika usiku chini ya ulinzi wa mabaunsa hao.
Alibainisha kuwa mkesha wa Januari 22 mwaka huu saa 7 usiku, mtuhumiwa alifika eneo hilo na mabaunsa wapatao 30 ambao walikuwa wakirandaranda, ili kusimamia umwagaji kifusi na kusawazisha, huku mmoja wa waporaji hao (jina tunalo) akiwa ameshikilia bastola.

No comments:
Post a Comment