Godfrey Nzowa. |
Raia 12 kutoka katika nchi mbili tofauti, wanashikiliwa Polisi kwa kukutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya heroin kilogramu 201, kupitia baharini.
Waliokamatwa ni raia wanane kutoka Iran wakati wengine wanne wakitoka Pakistan.
Akizungumza na mwandishi kwa njia ya simu, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Kikosi Maalumu cha Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya nchini, Godfrey Nzowa alisema kuwa watu hao walikamatwa juzi saa 6 usiku.
Alisema askari waliokuwa wakifanya doria ya kupambana na uhalifu baharini waliwakuta watu hao wakiwa katika eneo la kati ya Zanzibar na Dar es Salaam.
"Kweli kabisa hilo tukio lipo, hawa watu wamekamatwa kati ya Dar na Zanzibar wakiwa ndani ya jahazi na mzigo huo, haijulikani walikuwa wanaelekea wapi, mpaka tukishafanya mahojiano nao ndiyo tutafahamu yote hayo," alisema Nzowa.
Alisema inaonekana watu hao walikuja moja kwa moja kutoka Iran kwa kutumia meli na baadaye kubadilisha kutumia jahazi. Thamani ya dawa hizo bado haijafahamika mpaka baada ya mahojiano na watu hao.
"Kwa sasa tunawashikilia kwanza, thamani yake bado haijajulikana mpaka tutakapofanya nao mahojiano, pia kujua walikuwa wanatoka na kwenda wapi," aliongeza Nzowa.

No comments:
Post a Comment