Mojawapo ya aina za ving'amuzi. |
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, alisema hayo jana wakati akifunga mkutano wa jukwaa la kujadili mchakato wa kuhama kutoka analogia kwenda digitali, uliohusisha nchi zaidi ya 25 duniani.
"Bei za ving'amuzi ipo chini, japo sisi Serikali tunaona bado ipo haja tupunguze kodi zaidi ili ishuke chini zaidi kwa ajili ya kuwezesha kampuni nyingi kununua ving'amuzi hivyo na kuwauzia wananchi hasa walio vijijini," alisema.
Aidha alisema ni vizuri serikali ikiona vijana wamewezeshwa kujikusanya kwenye vikundi vyenye uwezo wa kutengeneza vipindi vya televisheni na makala, ili wajitengenezee fedha zao kiurahisi.
Alisema kuwa kabla ya Tanzania kuingia katika mfumo wa Digitali, wamiliki wengi wa Televisheni ndiyo waliokuwa wanatengeneza vipindi na makala mbalimbali kwenye vituo
vyao, lakini kwa sasa baada ya mfumo huo kuna fursa ya vijana kutengeneza wenyewe vipindi hivyo.
"Kilichopo hapa vijana wajiendeleze ili wawe na ujuzi wa kutengeneza makala na kuandaa vipindi, ambavyo vitatumika kwenye vituo vya televisheni na hatua hii itawawezesha vijana kupata fedha za kutosha,"alisema.
Aidha alisema moja ya maazimio katika mkutano huo waliyoona yapo haja ya kufanyiwa kazi ni pamoja na kupunguza bei ya televisheni ili wananchi wengi wamudu kuzinunua kwa ajili ya kujipatia habari za dunia zinazoendelea.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma alisema mfumo wa Digitali, umesaidia wananchi kwa upande wa simu za viganjani,
kuwasiliana na mtu yeyote kwa njia mbalimbali zilizoko kwenye simu hizo.
"Haya ni matunda ya digitali na maendeleo yamekuwa makubwa sana katika utumiaji wa simu hizi, kama vile wengi wanawasiliana kwa Whatsap, lakini kwa upande wa televisheni ni ngumu kidogo kuweza kuingia kwa maeneo yote kwa mara moja,"alisema.
Profesa Nkoma alisema walichofanya kuzima mitambo kwa awamu na sasa awamu ya pili, wanatarajia kwenda mikoa ya Morogoro, Tabora, Musoma, Mara na Dodoma na hatimaye
ifikapo Juni 2015 nchi nzima iwe katika mfumo wa digitali kama makubaliano ya Geneva yanavyosema.
Kuhusu uvumi wa kwamba mfumo huo unaua televisheni za zamani, alikanusha na kusema ni kitu cha kupuuza kwani hakina ukweli, sababu kitu kinachotakiwa ni kununua king'amuzi na unaendelea kuangalia vipindi vyako kama kawaida.
Pia, azimio walilotoka nalo katika mkutano huo ni kuhakikisha nchi zote za Afrika kuhakikisha zimeingia kwenye mfumo wa digitali kabla ya Juni mwaka 2015 kama walivyokubaliana katika mkutano wa Geneva, ambao ulitaka nchi zote duniani ifikapo mwaka huo ziwe dijitali.
No comments:
Post a Comment