Mzee Nelson Mandela akimfariji Jacob Zuma katika moja ya matukio miezi kadhaa iliyopita. |
Wakati shujaa wa demokrasia duniani, Nelson Mandela akiwa amezikwa tangu juzi, kura ya maoni nchini Afrika Kusini, inaonesha kuwa mrithi wake wa masuala ya siasa, Jacob Zuma ambaye ni Rais wa nchi hiyo, amepoteza uungwaji mkono, kutokana na tuhuma za kujitajirisha.
Utafiti ulioendeshwa na gazeti la The Sunday Times la nchini humo, unaonesha kuwa asilimia 51 ya wapiga kura waliosajiliwa ndani ya chama tawala cha ANC, wanataka Zuma ajiuzulu wakati akijitahidi kujaribu ‘kuvaa viatu’ vya Mandela.
Matokeo ya utafiti huo, uliofanywa na kampuni ya utafiti ya Ipsos, yamekuja katika wiki ambayo Zuma alizomewa katika ibada ya kumbukumbu ya Mandela, iliyofanywa katika uwanja wa FNB mjini Soweto Jumanne iliyopita.
Kati ya wapiga kura 1,000 wa ANC katika utafiti huo wa uwakilishi, asilimia 33 walisema hawako tayari kuipigia kura ANC kutokana na tuhuma, kwamba Zuma alitumia fedha za umma kuboresha hekalu lake akitumia dola milioni 20 za Marekani. Asilimia 42 walisema wanaamini ametumia vibaya fedha za walipa kodi.
Jumanne, Waafrika Kusini walimzomea rais wao katika ibada hiyo iliyohudhuriwa na maelfu ya watu kwa ajili ya kumkumbuka Mandela, ambaye urithi alioacha ni kutokuwa mchoyo na kujitolea.
Wengi wa waliozomea baadaye, walionesha wazi kutokubaliana naye lakini pia hasira dhidi ya anavyoendesha maisha yake wakati ambao Waafrika Kusini wengi wameendelea kuwa masikini, wasio na kazi wala makazi rasmi katika jamii ambamo watu wengi hawako sawa.
Mtangulizi wa Zuma, Thabo Mbeki, ingawa hakuwa maarufu sana wakati anaondolewa madarakani na Zuma mwaka 2008, alipokewa kwa shangwe alipoingia katika uwanja huo Jumanne.
Mbeki, ambaye alimrithi Mandela katika urais mwaka 1999, juzi aliukosoa utawala wa Afrika Kusini akihoji kama unaendesha mambo kwa viwango vya Mandela.
“Nadhani kusherehekea maisha yake vizuri kunahitaji kujiuliza swali juu ya ubora wa uongozi,” Mbeki aliuambia umati wa waombolezaji waliokuwa kwenye maombi ya Mandela jijini Johannesburg.
ANC chini ya Zuma imejikuta katikati ya mashambulizi juu ya madai ya kuendekeza udugu na rushwa. Chama hicho kinajiandaa kwa uchaguzi wa kitaifa mwakani.
Licha ya kutoaminika, lakini chama hicho kimeendelea kuwa na nguvu kikijivunia historia yake, kama chama mkombozi wa watu walionyanyasika kwa kipindi kirefu na bila shaka kitaendelea kuungwa mkono na wengi. Kuhusu kuzomewa kwa kiongozi wake, ANC imedai mazingira hayo yaliandaliwa na vyama vingine vya siasa.

No comments:
Post a Comment