Augustino Mrema. |
Mbunge wa Vunjo, Augustino Mrema (TLP), amesema atagombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015 katika jimbo hilo na kutoa hadhari kwa wanaolinyemelea.
Alisema hayo jana, wakati akichangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara kwa kipindi cha kuanzia Machi hadi Desemba 15 mwaka huu.
Alishukuru wabunge wenzake kwa kumjulia hali akiwa India kwa matibabu huku akisema kuna watu walijipitisha Vunjo kama vile jimbo hilo liko wazi wakidhani atakufa.
“Hafi mtu hapa, kwani kuna watu nilipokuwa napata matibabu walidhani nitakufa, wakaanza kujipitisha jimboni kwangu, nitaendelea kugombea katika uchaguzi ujao kwa kuwa afya yangu ni nzuri,” alisema.
Mrema (68) alisema hayo wakati juzi Mbunge wa Magu, Dk Festus Limbu, akitangaza rasmi kutogombea ubunge wa jimbo hilo katika uchaguzi huo.
Limbu alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuwa mbunge kwa miaka 15 ambayo ni awamu tatu na kuona ni vema kuwaachia wengine.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi Limbu ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba, alisema ni vema kuachia wabunifu wengine kuendeleza jimbo hilo, kwani kwa muda wote huo akiendelea kugombea, atakuwa akiendesha jimbo kwa mazoea tu.
“Miaka 15 si muda mfupi na sasa nimeona inatosha na kuamua kuwaachia wananchi wengine kuongoza jimbo hilo, kama nilikuwa na ubunifu katika kipindi hicho naamini kwa sasa nilichobakiza ni uzoefu peke yake, hivyo ni vema niachie wengine kwani wapo wenye uwezo kunishinda,” alisisitiza.
Limbu alisema mbunge ukiongoza awamu tatu na ukitaka kwenda awamu ya nne ni lazima ujipime na kuona kama utaweza kuendelea, kwani upo uwezekano wa watu wazuri kuliko wewe ni vema wajitokeze kwa maendeleo ya jimbo.
Alisema alipoingia ubunge katika jimbo hilo kulikuwa na kata zisizozidi tano lakini mpaka sasa anaondoka kukiwa na kata 18 na zote zina sekondari.

No comments:
Post a Comment