Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam. |
Mkazi wa Tabata Liwiti, Dar es Salaam, Maulid Mfaume (36) amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akiwa na pipi 83 za dawa za kulevya aina ya heroin, zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Sh milioni 64 zikiwa tumboni.
Kamanda wa Polisi wa Kikosi Maalumu cha Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya nchini, Godfrey Nzowa alisema jana kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi saa 8 kwenye uwanja huo.
Alikamatwa na kikosikazi cha uwanja huo, akitaka kusafiri kwa ndege ya Shirika la Ethiopia
kwenda China kupitia Ethiopia na Hong Kong.
Siku nne zilizopita watuhumiwa wengine wawili walikamatwa wakiwa na pipi 187 za heroin tumboni zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Sh milioni 135. Walikuwa wanawake wakisafiri kwa ndege ya shirika la Qatar kwenda China kupitia Hong Kong.
Kutoka Arusha inaripotiwa kwamba mkazi wa Ngaramtoni, Arumeru, Maryciana Kabunde (29) amekamatwa akiwa na magunia 26 ya bangi yenye uzito wa kilo 1,300.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberartus Sabas alisema jana kuwa mtuhumiwa ambaye ni mkulima alikamatwa juzi saa 4 asubuhi nyumbani kwake na bangi hiyo.
Alisema kukamatwa kwa Maryciana kulitokana na taarifa kutoka kwa raia wema ndipo polisi ilipokwenda kufanya upekuzi na kufanikiwa kukamata kiasi hicho cha bangi ambacho thamani yake haijajulikana.

No comments:
Post a Comment