Abiria kwenye stendi ya mabasi Ubungo. |
Hali ya usafiri katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo (UBT) imeanza kuwa ‘gumzo’, kutokana na wananchi wengi kujitokeza kituoni hapo, kukata tiketi zao kuelekea maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu.
Pamoja na hatua hiyo, Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) imewataka wamiliki wa mabasi kuendelea kuheshimu agizo la kutopandisha nauli kwa wananchi ili kuepuka kukumbana na adhabu ikiwemo kufungiwa.
Mwandishi alishuhudia mamia ya abiria, wakiingia na kutoka katika ofisi za kukatia tiketi kwa ajili ya huduma hiyo ya usafiri, ambapo pia Sumatra kupitia kwa Ofisa wake Mfawidhi Kanda ya Mashariki, Conrad Shio imetaka bei ya kila safari kutozwa kulingana na hadhi ya basi na viwango walivyoviweka.
“Tupo makini kuhakikisha abiria anatozwa fedha halali tuliyoiweka katika viwango vyetu. Hatutosita kumchukulia hatua mtu yoyote atayetoza nauli tofauti na tuliyoiweka katika viwango vyetu vya usafiri,” alisema Shio.
Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika ofisi hizo umebaini tatizo la mabasi mengi kukosa nafasi za kusafiri ndani ya siku tatu hadi nne zijazo kutokana na wananchi wengi kujitokeza kukata tiketi zao kwa nia ya kutaka kusafiri.
Katika ofisi za basi la Ndenjela, linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Dar es Salaam, mwandishi alishuhudia chati ya basi hilo ikiwa imejaa hadi Jumatatu ijayo.
Kwa mujibu mtu anayehusika na ukataji wa tiketi katika ofisi hiyo, ambaye hata hivyo hakupenda jina lake liandikwe, alisema hatua hiyo inasababishwa na wananchi wengi kutaka kusafiri kuelekea sehemu mbalimbali kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu.
“Ukweli hiki ni kipindi kigumu cha usafiri, ni wakati pia ambao kama abiria hatakuwa makini anaweza kujikuta anapoteza fedha zake kwa kulanguliwa na watu wasio waaminifu, mtu anaweza akakuambia basi fulani lina nafasi bila ukweli wowote akilenga umpatie fedha,” alisema.
Hata hivyo alisema tatizo la usafiri kituoni hapo linatarajiwa kuongezeka kadri siku zinavyozidi kwenda kutokana na mahitaji ya usafiri kuongezeka.
Mbali na basi hilo pia mabasi mengi yanayoelekea Mwanza, Arusha, Kilimanjaro na Bukoba pia yalishushudiwa yakikosa nafasi ya kusafiri kwa zaidi ya siku mbili zijazo kutokana na abiria wengi kujitokeza kukata tiketi zao mapema.

No comments:
Post a Comment