![]() |
| Luteni Rajab Mlima. |
“Ameoa leo, amenioa leo, hii ndiyo harusi yangu!” Ni kilio cha Luteni Asia, mchumba wa Luteni Rajab Mlima, askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) aliyeuawa na waasi wa M23 akiwa vitani Goma, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Luteni Asia ambaye alikuwa miongoni mwa ndugu waliofika katika viwanja vya Jeshi vya Lugalo, Dar es Salaam jana kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu, kilio chake cha uchungu kilifanya baadhi ya wanajeshi wenzake waliokuwa wanamfariji kutokwa machozi.
“Jamani hii ndiyo harusi yangu leo, amenioa leo…amenioa leo…labda Mungu ana mipango yake,” alipaza sauti ya uchungu mwanadada huyo ambaye alitarajia kuanza mwaka mpya akiwa katika maisha ya ndoa na mchumba wake Mlima.
Asia ambaye alikuwa amevaa pete yake ya uchumba, ndoto yake hiyo imekatika ghafla baada ya mchumba wake Luteni Mlima (36) maisha yake kukatishwa kwa risasi ya waasi wa M23.
Wakati Asia akitarajia kuanza maisha mengine mapya, kwa mtoto wao Zuruhafi hali ni tofauti. Yeye kilio chake ni kumpoteza baba kipenzi na sasa hajui maisha yake yatakuwaje duniani bila mzazi wake huyo wa kiume.
Zuruhafi (10) ndiye mtoto pekee wa marehemu Mlima, ambaye amekutwa na mauti bila kuingia kwenye ndoa; lakini alijaaliwa mtoto huyo wa kike.
“Baba wamemwua, wamempiga risasi kwa bastola, jamani nitakwenda wapi mimi!” Mtoto huyo mdogo alisikika akilia huku amekumbatiwa na ndugu za marehemu baba yake, ambao nao hawakuwa wanajiweza kutokana na tukio hilo la ghafla.
Luteni Mlima ambaye aliondoka nchini Juni mosi na kwenda DRC viliko vikosi vya JWTZ vikishiriki kulinda amani, kabla ya safari yake alimwahidi Asia na mtoto wao kuwa angerejea nchini Desemba kwa ajili ya kufunga ndoa.
Lakini hali imekuwa tofauti, kwa Asia, Zuruhafi na ndugu wengine badala ya kwenda kumpokea uwanja wa ndege mpendwa wao akiwa hai na mwenye bashasha, ilikuwa tofauti kwa kumpokea akiwa kimya ndani ya jeneza.
Mdogo wa marehemu, Shaibu Mlima aliliambia gazeti hili kuwa vikao vya harusi ya kaka yake na Asia vilishakusanya fedha kwa ajili ya maandalizi ya harusi hiyo ambayo ilikuwa ifungwe Desemba 28.
“Tulishakaa vikao vingi na fedha zilishakusanywa na tulibakiza vikao vitatu vya maandalizi ya harusi ya ndugu yangu; harusi yenyewe ilipangwa iwe Desemba 28. Tunasikitika hatua hiyo haikufikiwa, hatuna cha kusema Mungu mwenyewe alipanga hivyo,” alisema Shaibu.
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Samwel Ndomba, aliwaambia waombolezaji viwanjani hapo kuwa Mlima alipoteza maisha wakati akitelekeza majukumu yake ya ulinzi nchini DRC jambo ambalo alikuwa analifanya kwa ukakamavu.
“Alitekeleza majukumu yake kwa ujasiri na uhodari, kitendo ambacho kimeendelea kuiletea nchi na Jeshi letu heshima mbele ya Jumuiya ya Kimataifa,” alisema Luteni Jenerali Ndomba.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, alisema Taifa limepoteza ofisa wa Jeshi katika kipindi ambacho alikuwa anahitajika sana hasa kwa kutoa ulinzi kwa ndugu zetu wa jimbo la Goma DRC.
“Damu yake haitamwagika bure, tutaendelea kutetea ndugu zetu wa DRC kwa kulinda amani ndani ya nchi hiyo hadi amani ya kweli itakapopatikana,” alisema.
Alisema Serikali inawapa pole wanafamilia na kuahidi kuwa ofisi yake itaendelea kuwa nao bega kwa bega katika kipindi hiki na baada ya msiba.
Luteni Mlima alipigwa risasi na kufa Agosti 27, mjini Goma wakati akitoa ulinzi kwa kuwakinga raia wasidhurike na mapigano katika eneo la Kiwanja, kwenye mlima wa Gavana wakati wa mapambano kati ya majeshi ya DRC na waasi wa M23.
Huyo anakuwa ofisa wa pili wa JWTZ kuuawa katika mapigano nchini humo, baada ya ofisa mwingine wa cheo cha meja kuuawa kwa bomu lililorushwa na waasi hao katika mapigano makali yaliyotokea katika mji huo wa Goma, Agosti 28.
Meja Khatib Mshindo, aliuawa baada ya kujeruhiwa na bomu hilo akiwa kazini na akavuja damu nyingi wakati akikimbizwa hospitalini.
Wakati Mshindo aliyekuwa miongoni mwa askari wa Tanzania wanaounda Jeshi la Umoja wa Mataifa akifikwa na mauti, wapiganaji wengine 10 walijeruhiwa.
Mwili wa marehemu Meja Mshindo ulisafirishwa siku iliyofuata
kupelekwa Entebbe, Uganda ambako ulifanyiwa matayarisho ya mwisho kabla ya kuletwa nchini kwa maziko.
Kuuawa kwa askari huyo kulikuwa kumekuja siku 47 tu tangu kuuawa kwa askari saba wa Tanzania waliokuwa wakilinda amani katika jimbo la Darfur Sudan na kikundi cha Janjaweed. Luteni Mlima alizikwa jana katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.

1 comment:
Hii historia imeniuma sana mara baada ya kusoma siku ya tarehe 28.12 marehemu alitarajia kufunga pingu za maisha na mwandani wake bi Asia,ambapo mm nasherehekea siku yandoa yangu,jamani hamna kitu kinachouma kama hiki kutotimiza ndoto,ila mungu ana makusudi yake dada Asia jipe moyo na mkumbuke mtarajiwa wako kwa maunganisho aliyokuachia yaani uliyonayo wewe na yy ambayo ni mtoto alokuachia,Mungu alitoa na ametwaa,ww ama cc tulimpenda lakini mungu amempenda zaidi,mwanga wa milele amwangazie na siku utakutana naye huko mbele ya Safari (ahera kwani cc wote ni wakurudi mavumbini),POLE SANA BIBIE ASIA ;MTOTO NA WAFIWA WA AKRIBU WOTE,Mdau kutoka Ujerumani
Post a Comment