Saturday, November 2, 2013

BINTI ACHINJWA HADI KUFA BAADA YA KUBAKWA NA KUNDI LA WANAUME...

Mamia ya waombolezaji wakiwa wamefurika kanisani katika misa ya kuombea mwili wa binti huyo.
Mauaji ya kutisha ya binti wa miaka 17, ambaye alibakwa na kundi la wanaume, kukatwa kichwa kwa namna ya kutisha na kutelekezwa akikata roho kwenye eneo la jengo, yamelipua makelele kila kona nchini Afrika Kusini.

Anene Booysen aligunduliwa na walinzi katika eneo hilo lililoko kwenye mji uliodorora wa Bredasdorp, maili 80 mashariki mwa Cape Town.
Kwa mujibu wa msemaji wa Idara ya Afya, majeraha yake yalikuwa makubwa mno kiasi familia yake kuzitaka mamlaka kutoelezea.
Hatahivyo baadaye ilibainika kwamba tumbo lake lilikuwa limechanwa hadi kwenye sehemu zake za siri na kwamba alifariki kutokana na majeraha yake hayo hospitalini.
Alimudu kumtambua mmoja wa washambulizi wake kabla ya kufariki na wanaume wawili wamefikishwa mahakamani kwa mashitaka ya kubaka na kuua.
Jonathan Davids, miaka 22, na Johannes Kana, miaka 21, walifunikwa sura zao dhidi ya kamera za televisheni na wapigapicha wakati wakiwa njiani kuingia katika chumba cha mahakama.
Hakimu aliamuru watuhumiwa hao wawili kubaki gerezani hadi Februari 26 pale maombi yao ya dhamana yatakaposikilizwa. Wanakabiliwa na kifungo cha maisha jela endapo watapatikana na hatia.
Polisi walimwachia mtu wa tatu aliyekamatwa baada ya tukio hilo kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha kumwingiza kwenye uhalifu huo, lakini walisema walikuwa wakichunguza kujua kama kulikuwa na wengine pia waliohusika.
Umati wa watu 100 uliandamana nje ya chumba hicho cha mahakama huko Bredasdorp, wakiwa wamebeba mabango yanayosema 'Usioneshe huruma kwa wabakaji' na 'Hakuna dhamana kwa wauaji'.
Kaka wa Booysen alivieleza vyombo vya habari vya mjini humo alimfahamu mmoja wa watuhumiwa hao.
Alisema: "Alikuwa rafiki yangu, tulisoma shule pamoja, tuliishi kwenye nyumba moja, tulikuwa kama ndugu."
Ijumaa, mamia ya watu waliandamana mjini Bredasdorp, wakiimba 'imetosha' na mamia walihudhuria mazishi siku ya Jumamosi.
Mamia ya waombolezaji, wakiwamo wanasiasa, walifurika kwenye kanisa moja katika mji wa Bredasdorp, ambapo turubai liliwekwa kwa ajili ya  wote waliokosa nafasi ndani.
Mauaji hayo yameakisi tukio la ubakaji wa mwanafunzi kwenye basi New Delhi mwaka jana, na limelenga umakini katika kiwango cha juu cha makosa ya ubakaji nchini Afrika Kusini.
Booysen alikutwa na walinzi akiwa amelala umbali mfupi kutoka nyumbani kwake baada ya kusherehekea kwenye baa moja jioni ya Ijumaa iliyopita.
Mnamo Jumamosi, vyombo vya habari vya Afrika Kusini viliripoti polisi imemkamata mchungaji mmoja wa Johannesburg kwa kumshawishi mwanamke mmoja ndani ya kanisa lake na kumbaka.
Afrika Kusini ina idadi ya juu ya ubakaji ulioripotiwa kwa kichwa cha idadi ya nchi yoyote mwanachama wa Interpol, huku mengi zaidi ya 64,500 yakiwa yameripotiwa mwaka 2011/2012.
Ubakaji unasemekana kufanyika nchini Afrika Kusini kila baada ya dakika nne.
Hata pale watuhumiwa wanapokamatwa, asilimia 12 tu ya kesi huishia kwa kutiwa hatiani na uhalifu wa ubakaji mara chache umevuta hisia kubwa za jamii.

No comments: