![]() |
| Profesa Mark Mwandosya. |
Waziri asiye na Wizara Maalum, Profesa Mark Mwandosya amesema kuwepo ama kutokuwepo kwa mawaziri na watendaji wengine bungeni, si kikwazo cha utekelezaji wa uamuzi wa Bunge, kwa kuwa daima Serikali inafanyakazi kwa pamoja na inaheshimu mawazo ya wabunge.
“Napenda mtambue kuwa kuwepo ama kutokuwepo waziri bungeni si tatizo, Serikali inafanya kazi kwa taarifa, tunathamini sana maoni ya wabunge, macho na masikio ya Serikali wakati huu wa Mkutano wa Bunge yanaelekezwa Dodoma, hivi ninavyozungumza kuna luninga katika kila Idara ya Serikali na hata Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Naibu wake, wanasikiliza majadiliano haya,” alisema Profesa Mwandosya.
Alitoa kauli hiyo jana baada ya juzi Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuwaonya mawaziri kuhusu mahudhurio hafifu katika majadiliano ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Serikali wa Mwaka 2014/2015.
Wabunge pia jana wakati Bunge lilipokaa kama Kamati kujadili mapendekezo ya mpango huo, walihoji kuhusu mahudhurio ya mawaziri, manaibu wao na watendaji wengine wa Serikali wakiwemo makatibu wakuu baada ya kuwepo mawaziri wasiozidi saba bungeni kati ya mawaziri 29.
Walisema kutokuwepo kwa watendaji hao bungeni wakati wabunge wakitoa mapendekezo kuhusu mpango huo, ni dharau na kikwazo cha utekelezaji ingawa kumekuwa na mipango mizuri, inakwamishwa na watendaji.
Akifafanua, Profesa Mwandosya alisema wapo maofisa bungeni wanaoandika kila maoni na kwa kuwa sasa macho yote yanaelekezwa Dodoma, mawaziri waliopo wanasikiliza kwa niaba ya wenzao.
“Si kwamba nahalalisha kutokuwepo kwao, ni vizuri kuwepo ila pale penye sababu ya msingi inakuwa hivi ila tunashirikiana katika hili,” alisema Profesa Mwandosya.
Wabunge waliohoji utoro wa mawaziri katika mjadala huo, waliposimama kuchangia mapendekezo ya Serikali kuhusu mpango huo wa maendeleo ni Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Mchungaji Peter Msigwa, Iringa Mjini (Chadema), Mbunge wa Mgogoni, Kombo Hamis Kombo (CUF) na Mbunge wa Mbarali, Modestus Kilufi (CCM).
Mbatia alisema, “tunazungumzia suala la maendeleo ya Taifa kuna mawaziri kamili wanne tu hapa kati ya mawaziri 29, ni kama kuma mchokomchoko fulani, kurasa 62 za mapendekezo, 47 zina mambo ya mwaka jana na zilizobaki ndio angalau yanajadilika, sidhani kama tutafika kwa hali hii.”
Mchungaji Msigwa alishangaa ‘utoro’ wa mawaziri wakati walipaswa kuwepo katika majadiliano, kutokana na kile alichokieleza kuwa wao kama Serikali ndio wasimamizi na watekelezaji wa mpango.
“Hata mkijitetea hampo kabisa, mko wapi?” Alihoji Msigwa wakati mawaziri waliokuwepo na baadhi ya wabunge wa CCM walipokuwa wakinong’ona chini chini alipokuwa akichangia.
“Kuna utaratibu wa kusema bila kutenda, hii ndio shida kubwa, pamoja na agizo la Spika la jana (juzi), leo hawapo hao mawaziri, hapa walipaswa kuwepo mawaziri, naibu wao na makatibu wakuu, nani atatekeleza na kufanyia kazi maoni yetu, hii dharau na mchezo wa kuigiza,” alisema Kombo.
Spika wa Bunge, Anne Makinda alipokuwa akiahirisha Bunge juzi, aliwataka mawaziri wote kuwepo kwa kuwa mpango huo, unahusu wizara zote, hivyo wangelazimika kila mmoja kuzungumzia na kufafanua eneo lake badala ya kumwachia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wasira.
“Kila waziri anapaswa awepo, huu si mpango wa waziri anayehusika na Mipango (Wasira) pekee, majibu mnayo ninyi, hivi sasa tunashauri lakini mwisho tutasema kama Bunge, mjue tu kwamba uwepo wenu si mzuri,” alisema Spika juzi.

No comments:
Post a Comment