Sunday, November 17, 2013

IMEFICHUKA!! 'MJANE MWEUPE' SAMANTHA ALIAMURU KUUAWA KWA ABOUD ROGO NA WENGINE SITA...

KUSHOTO: Samantha Lewthwaite. KULIA: Aboud Rogo Mohammed.
'Mjane Mweupe' mkimbizi wa mhusika wa tukio la ulipuaji mabomu la 7/7 anasakwa kwa kuhusiana na mauaji ya watu saba nchini Kenya, polisi wamefichua.

Mzaliwa wa Uingereza, Samantha Lewthwaite anatuhumiwa kuamuru mauaji hayo ya viongozi wawili wa Kiislamu, wahubiri wawili wa Kiprotestanti, na wengine watatu wanaohusiana na kundi la kigaidi la al-Shabaab.
Maofisa usalama wa Kenya wamemwelezea mjane huyo kama 'tishio la kushangaza' na kusema wanafanya kazi 'masaa 24' kuweza kumkamata.
Mhubiri kisirani Aboud Rogo Mohammed alipigwa risasi barabarani wakati akimpeleka mkewe hospitali Agosti 27, mwaka jana.
Rogo alipigwa risasi mara 17 wakati akiendesha gari sambamba, wakati mkewe Khania Said alipigwa risasi mara moja pajani. Baba yake na binti yake mwenye miaka mitano, ambao pia walikuwamo kwenye gari hilo hawakupigwa risasi.
Samantha alikuwa mfuasi wa Rogo na alihubiri naye katika msikiti wa Masjid Musa katika mji wa Mombasa, na kuwabadili maelfu ya Wasomali kujiunga na al-Shaabab katika mapambano.
Hatahivyo, wawili hao walifarakana na vita ya maneno ikaanza, wakati ambapo Rogo alitoa wito wa 'kujichunga' na Samantha, ambaye ageuka na kuwa na matakwa makubwa mno. Aliuawa miezi tisa baada ya mjane huyo kuonekana mara ya mwisho.
Mrithi wake, Sheik Ibrahim Rogo, alikumbana na mkasa kama huo mwezi uliopita pale alipouawa pia katika makimbizano ya magari sambamba na washirika wake Omar Abu Rumeisa, Salim Aboud na Gadafi Mohammed.
Mauaji hayo yamedhihirisha mpasuko kati ya al-Shabaab na Samantha, huku vyanzo kutoka vikosi vya usalama vikisema kuna msuguano wa nguvu kati ya viongozi wa kikabila na Mjane huyo Mweupe.
Mwanaintelijensia mmoja alisema katika mahojiano: "Samantha Lewthwaite anapigania udhibiti mkubwa wa al-Shabaab ambao unachukiza utawala msonge wa taasisi hiyo.
"Amekuwa mwenye wazimu na asiyeaminika kwenye kundi hilo baada ya kuwa mafichoni kwa muda mrefu mno. Wanaamini hukumu yake imesongwa na anaweza kujikuta akijiengua mwenyewe hivi karibuni."
Wachungaji wawili wa Kiprotestanti, Charles Matole na Ebrahim Kidata, pia wanaaminika kuuawa kwa matakwa ya Samantha.
Mwili wa Matole, miaka 41, ulikutwa katika kanisa la Redeemed Gospel mjini Mombasa mnamo Oktoba 19 akiwa ameketi kwenye kiti na kukumbatia Biblia.
Aliuawa kwa kupigwa risasi moja kichwani baada ya polisi kumhoji kuhusiana na iwapo kuna kijana yeyote alifika kwake kuomba msaada baada ya kuwa ametakiwa kujiunga na al-Shabaab.
Mwili wa Kidata ulikutwa umetupwa kwenye vichaka katika mji wa Kilifi, maili 40 kutoka Mombasa, siku moja kabla ya kuuawa Matole.
Mhubiri huyo mpya wa Makanisa ya Kipentekoste Afrika Mashariki, anaaminika kuwa alinyongwa.
Kamanda wa Polisi wa East Kenya, Aggrey Adoli alisema: "Tunaamini Samantah Lewthwaite anahusika na mauaji haya pamoja na makundi ya wengine.
"Tunaamini anahusika katika kuajiri wanajihadi na wanaharakati wa al-Shabaab na Al-Qaeda nchini humu na wengine binafsi. Tutakapomkamata Samantha Lewthwaite atakuwa na maswali mengi ya kujibu.
"Bila shaka ni tishio la ajabu kwa taifa na usalama wa kimataifa. Tunafanya kazi masaa 24 kuweza kumkamata kumkomesha kufanya umwagaji zaidi wa damu."
Ofisa huyo alisema anasakwa kwa mashitaka ya 'mauaji na kuwaingiza vijana wa Kiislamu katika ghasia'.
Wafuasi saba wa Samantha, wakiwamo Mhubiri wa Kitanzania, raia wa Somalia, raia wa Uganda na Wakenya watatu, pia wamekuwa wakisakwa vikali.
Samantha ni mjane wa gaidi aliyejilipua 7/7 Germaine Lindsay, ambaye alijilipua katika treni ya Piccadilly Line kati ya stesheni za King's Cross St Pancras na Russell Square.
Mama huyo wa watoto wanne alizaliwa huko Aylesbury, Buckinghamshire, na ni mtoto wa mwanajeshi wa zamani kabla ya kubadili dini na kuwa Muislamu.
Mjane huyo anahusishwa na mauaji ya halaiki katika jengo la Westgate Mall mjini Nairobi ambapo watu 67 walipoteza maisha, na inadhaniwa kuwa amejificha nchini Somalia.
Interpol ilitoa waranti ya kukamatwa muda mfupi baada ya mashambulio ya kigaidi mjini Mombasa mnamo mwaka 2011.

No comments: