Thursday, October 17, 2013

UCHUNGUZI SASA WAFICHUA YASSER ARAFAT ALIUAWA KWA MIONZI YA SUMU...

Yasser Arafat (kushoto) na mkewe, Suha.
Kiongozi wa zamani wa Palestina, Yasser Arafat inawezekana aliuawa kwa sumu yenye nururishi ya polonium, wanasayansi nchini Uswisi wamefichua.

Arafat alifariki nchini Ufaranza Novemba 11, 2004, akiwa na umri wa miaka 75, lakini wakati huo madaktari hawakuweza kubainisha sababu ya kifo.
Wataalamu wamefichua kwamba mali kadhaa  na vitu vya nguo mali za Arafat, vikiwamo mswaki wake, kofia na nguo ya ndani, vilikuwa na 'viwango vya juu visivyoelezeka' vya nyenzo za nururishi hizo.
Nyenzo hizo ni sawa na zile zilizotumika kumuua shushushu wa zamani wa Urusi, Alexander Litvenenko mjini London mwaka 2006.
Arafat, ambaye alifariki baada ya kuugua kwenye makao makuu yake yaliyoko katika Ukanda wa Magharibi, alionesha dalili za kichefuchefu, maumivu ya tumbo na figo na ini kushindwa kufanya kazi - ishara zinazopatikana kwa aliyeathirika na sumu ya mionzi.
Lakini upungufu wa upotevu wa nywele au upungufu wa uboho unaibua mashaka katika nadharia hiyo, wanasayansi hao wanayoiafiki.
Uvumi mwingi umezingira kifo cha Arafat baada ya madaktari kushindwa kutambua jinsi alivyokufa.
Hisia zimeanzia kutoka kwa wanaokashifu kwamba alifariki kutokana na virusi vya ukimwi hadi madai kwamba wapinzani wake walimwekea sumu.
Ubashiri umeendelea kwa nguvu ileile wakati mjane wake Suha mwanzo alipokataa kufanyika uchunguzi wa mwili wa mume wake.
Lakini alibadili mawazo yake na kuwataka majaji nchini Ufaransa mwaka jana kuanzisha uchunguzi wa mauaji kuhusiana na kifo cha mumewe, akidai aliwekewa sumu sababu alikuwa 'kikwazo cha amani'.
Wataalamu katika taasisi ya Lausanne's Radiation Physics Institute sasa wametoa hadharani taarifa za vipimo hivyo ambavyo 'vinashawishi uwezekano' kwamba hakufa kifo cha kawaida.
Taarifa hiyo ilisema: "Vipimo kadhaa kwenye sampuli za majimaji ya mwilini vilikuwa na kiwango cha juu kisichoelezeka cha polonium 210, kulinganisha na sampuli dhibiti.
"Hivi vilivyopatikana vinachochea uwezekano wa Arafat kuuawa kwa sumu ya polonium 210."
Walichunguza vitu 37 vya mavazi ya Arafat na kulinganisha viwango vya polonium na idadi sawa ya vitu safi.
Mivurumisho ya kompyuta, ambayo inakadiria kasi ambayo nyenzo za nururishi hizo zinapovunjika, zinaashiria kwamba kiwango cha polonium 210 kinaweza kuwa kile kile cha 'kilichomezwa' mwaka 2004.
Timu hiyo, ambayo ugunduzi wao umechapishwa kwenye jarida la tiba la Uingereza The Lancet wiki hii, ilisema wanasikitika kwamba hakukuwa na uchunguzi wowote wa mwili uliofanyika baada ya kifo cha Arafat.
Polonium huvunjika haraka kwenye mwili wa binadamu na ni vigumu kugundua kama kuna ucheleweshaji wowote.
Wachunguzi hao waliongeza: "Upelelezi huo unaweza kuwa wa muhimu katika kesi hii sababu japo nguvu ya sumu ya polonium inaweza kutobainishwa wakati wa utaratibu huo, sampuli za mwili zinaweza kuwekwa na kuchunguzwa baada ya hapo."
Mwanasheria wa mjane wa Arafat, Pierre-Olivier Sud alivieleza vyombo vya habari vya Ufaransa mwaka jana: "Suha Arafat anaamini kwamba mamlaka husika zitaweza kubaini mazingira hasa ya kifo cha mumewe na kufichua ukweli huo, hivyo haki kuweza kupatikana.
"Yeye na familia yake wanataka ukweli na si kingine bali ukweli huo. Hakuna swali la itikadi yoyote au utumiaji siasa."
Mjane wa Arafat pia alikieleza kituo cha televisheni cha Al Jazeera mnamo Julai 2012 kwamba wote Marekani na Israeli walimchukuliwa mumewe kama 'kikwazo cha amani'.
Aliongeza: "Nataka dunia ijue ukweli kuhusu kuuawa kwa Yasser Arafat."
Arafat alikuwa amewekwa kizuizini na Israeli kwenye makao makuu yake mjini Ramallah wakati alipougua mnamo Oktoba 2004.
Baadaye alipewa ruhusa ya kupelekwa kwenye hospitali ya kijeshi ya Percy karibu na Paris, akiwaeleza wasaidizi wake kabla hajaondoka: "Kwa mapenzi ya Mungu, nitarejea."
Lakini chini ya kipindi cha mwezi mmoja baada ya kuwasili, akawa mahututi na kufariki Novemba 11, 2004.
Madaktari waliomtibu walisema wakati huo inawezekana kuwa alikufa kutokana na kuganda kwa damu na kutupilia mbali madai ya kulishwa sumu.
Wakati Wapalestina wakisema kwamba ushahidi wowote kwamba Arafat alilishwa sumu utamaanisha kwamba Israeli inahusika kwa namna fulani, msemaji wa Serikali ya Israeli amepuuza madai hayo.

No comments: