Thursday, October 17, 2013

RUNDO LA VIFAA LAANGUKA KUTOKA KWENYE NDEGE YENYE ABIRIA 148 ANGANI...

Ndege hiyo aina ya 787 Dreamliner baada ya kutua.
Rundo la vifaa vya kuendeshea imeanguka kutoka kwenye ndege moja katikati ya safari na kuacha tundu kwenye ndege hiyo huku ikiwa na abiria 148 ndani yake.

Uchunguzi umeanzishwa baada ya vifaa hivyo kudondoka kutoka kwenye kiunzi cha ndege hiyo ya Air India 787 Dreamliner Jumamosi iliyopita.
Hili ni tukio la karibuni kabisa katika mfululizo wa ajali tangu ndege hiyo ya teknolojia ya juu kuzinduliwa miaka miwili iliyopita.
Boeing ilisema kupotea kwa sehemu kubwa ya kiunzi hicho haikusababisha hatari yoyote kwa usalama wa abiria.
Ndege hiyo ilikuwa imebeba watu 148 wakiwamo wafanyakazi wa ndege hiyo katika ndege iliyokuwa ikitokea Dubai kuelekea Bangalore, imeripotiwa.
Marubani hawakugundua sehemu hiyo kubwa ya vifaa yenye ukubwa wa futi nane kwa nne haikuwapo hadi baada ya ndege hiyo kutua, kuongeza kwamba mamlaka za usalama wa anga nchini India zinafanya uchunguzi.
Boeing ilisema sehemu hiyo kubwa ya vifaa vilivyopotea ilianguka kutoka upande wa chini wa ndege hiyo katika upande wa kulia.
Picha inaonesha uwazi mkubwa wenye vifaa na muundo wa ndege hiyo ukionekana ndani.
Msemaji wa Boeing, Doug Alder alisema wanashughulikia kujua kilihosababisha sehemu hiyo kubwa ya vifaa kuanguka na kukataa kusema kama ndege hiyo ilitengenezwa katika kiwanda cha Boeing cha South Carolina.
Idadi kubwa ya ndege za Air India zimetokea kwenye kiwanda hicho cha kuunganisha ndege.
Kwa mujibu wa ripoti, sehemu hiyo kubwa ya vifaa ilibadilishwa na vingine kutoka kwenye ndege nyingine ya 787 Dreamliner iliyokuwa imetoka kukabidhiwa ambayo haikuwa imefikisha muda wa kufanyiwa ukarabati.
Inaaminika kwamba ndege hiyo sasa inasubiria vipuri.
Matatizo kwenye ndege hiyo ya 787 ni pamoja na betri kupata moto na kuwashawishi wadhibiti kuzuia kundi zima mnamo Januari.
Ndege hizo ziliruhusiwa tena Aprili. Mnamo Julai, moto ulilipuka kwenye ndege tupu iliyokuwa imeegeshwa kwenye Uwanja wa Heathrow.
Wiki iliyopita tu Dreamliners mbili zililazimika kufuta safari ndani ya masaa 24 sababu ya matatizo tofauti ya kiufundi kwenye vyoo na mfumo wa upoozaji barafu.
Shirika la ndege la Japan lililazimika kurejesha ndege yake yenye makazi yake mjini Tokyo kutoka Moscow jana kutokana na matatizo kwenye vyoo vya ndege hiyo.
Msemaji wa shirika hilo, Takuya Shimoguchi alisema hitilafu za vyoo hivyo inaweza kuwa ilisababishwa na matatizo ya umeme.
Ndege nyingine ainaya ya Dreamliner ya shirika hilo la Japan ilibadilishwa uelekeo kwenda San Diego sababu ya uwezekano wa hitilafu kwenye mfumo wa ugandishaji barafu.

No comments: