![]() |
| Jaji Joseph Warioba. |
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeiagiza Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kutumia fedha zilizotengwa kwa ajili ya kupangisha ofisi, kuilipa pango Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ili imalize deni linalodaiwa la Sh bilioni 1.2 na mkandarasi.
Deni hilo linatokana na ujenzi wa jengo la ghorofa nane mali ya wizara hiyo, ambalo sasa linatumiwa na Tume hiyo, lakini tangu ipangishe, haijawahi kulipa kodi inayotakiwa.
Agizo hilo lilitolewa na Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Abdul Marombwa, baada ya kupokea malalamiko kuhusu deni hilo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abduwakil.
Akizungumza mbele ya kamati hiyo, Abdulwakil, alisema kwa sasa wizara hiyo inakabiliwa na tatizo la deni hilo, ambalo linatokana na jengo hilo linalotumiwa na tume hiyo ya Katiba, huku wizara ikiwa haina uwezo wa kulilipa kwa kuwa hawajapatiwa fedha yeyote na Wizara ya Katiba na Sheria, tangu tume hiyo ihamie kwenye jengo hilo.
“Jengo linalotumiwa na hii tume hatujalipa fedha zake kwa mkandarasi hadi leo, na tayari ametishia kusitisha huduma za jengo iwapo hatalipwa, akifanya hivyo itakuwa ni aibu kubwa, tunaomba hawa wenzetu watusaidie kulipa kwa kuwa kwa sasa bajeti yetu ni ndogo,” alisema.
Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kabwe Zitto, alisema haiwezekani Bunge lipitishe bajeti ya Tume hiyo ya Katiba ikiwa na fedha zilizotengwa kwa ajili ya kukodisha ofisi halafu fedha hizo zitumike kwa masuala mengine.
“Sasa naagiza fedha zilizopitishwa na Bunge kwa ajili ya kulipia pango kwa Tume zianze mara moja kulipwa kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili na wao wamalize deni lao,” alisisitiza Marombwa.

No comments:
Post a Comment