![]() |
Ufoo Saro akiwa kitandani hospitalini. |
Akizungumza na mwandishi jana, Ofisa Uhusiano wa hospitali hiyo, Aminieli Aligaesha alisema hali ya mwandishi huyo inazidi kuimarika, lakini bado anatakiwa kuendelea kupumzika zaidi.
“Ufoo, hali yake kwa sasa ni nzuri, anazungumza na anatambua watu lakini kwa sasa haturuhusu watu kumtembelea isipokuwa ndugu zake tu kwa sababu anatakiwa kupumzika zaidi… nafikiri ataruhusiwa watu kumtembelea baada ya siku mbili au tatu kuanzia sasa,” alisema.
Ufoo alijeruhiwa kwa risasi Jumapili asubuhi na mzazi mwenzie, Anthery Mushi, nyumbani kwa mama yake, Anastazia Saro aliyepigwa pia risasi na kufa papo hapo. Pia mwanaume huyo alijiua.
Baada ya tukio hilo, Ufoo alipelekwa katika hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha, ambapo baadae alihamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili na kufanyiwa upasuaji, ambapo kwa sasa anaendelea vyema.
No comments:
Post a Comment