KOMPYUTA ZA BUNGE ZATUMIKA KUPERUZI TOVUTI ZA NGONO MARA 300,000...

Moja ya picha chafu za ngono.
Wabunge na wafanyakazi wao walifungua tovuti za ngono mara 300,000 kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita, rekodi rasmi zimefichua.

Jumla hiyo - ambayo inawakilisha zaidi ya tovuti 820 kwa siku - ilitolewa na mabosi wa mitandao wa Palace of Westminster juzi katika kutekeleza ombi la  uhuru wa habari.
Takwimu hizo zinatanda 'majaribio ya kufungua tovuti zilizotengwa kama za ngono'. Hatahivyo mfanyakazi wa Bunge alisema ilijumuisha pop-ups na hivyo haiakisi juhudi za makusudi za kutafuta taarifa za ngono.
Machine zote zinazodhibitiwa ziliunganishwa kwenye mtandao wa Bunge, ambao unatumiwa na wabunge na wafanyakazi wao, kati ya majira ya joto ya mwaka 2012 na 2013.
Kulikuwa na tofauti pana katika takwimu kwa mwezi - kukiwa na majaribio 114,844 kutazama picha za ngono zilizotengenezwa Novemba, lakini 15 tu katika mwezi Februari.
Matthew Sinclair, mtendaji mkuu wa muungano wa walipakodi, alisema: "Hii inaakisi ukweli kwamba watu wengi wanaofanya kazi katika Bunge wanatumia muda mwingi mno kwenye tovuti kwamba hawana kazi za kufanya.
"Intaneti inaweza kuwa silaha nzuri kwa Wabunge na wafanyakazi wao pale inapotumika kungalia kwa makini utungaji sheria wa serikali. Hatahivyo walipakodi wanatarajia wabunge wao na wote wanaofanya kazi kwenye ofisi zao kufanya kazi zao muhimu badala ya kutumia muda kuperuzi tovuti zenye kuleta utata."
Msemaji wa Bunge alisisitiza rekodi hizo hazithibitishi watumiaji 'walikusudia' kutazama ngono, na alisema Bunge halitoweka kanuni zitakazozuia majaribio 'kufanya utafiti'.
Aliongeza: "Hatutazitilia maanani data hizo kutoa uwakilishi sahihi wa idadi ya majaribio ya makusudi yaliyofanya na watumiaji mitandao kutokana na njia ambazo tovuti zinaweza kusanifiwa kwa ajili ya matumizi."
Mapema mwaka huu ilifichuliwa kwamba Wabunge na wafanyakazi wao wamekuwa wakipoteza maelfu ya masaa katika mwaka wakihangaika na kurasa zao za Facebook, kucheza michezo ya kompyuta na kucheza kamari za mitandaoni. Rekodi rasmi zinaonesha eneo la Bunge lilifungua Facebook hadi mara milioni 3 kwa mwezi - mara 300 zaidi kulinganisha na walivyotazama tovuti ya BBC News.

No comments: