BABA ALIYEMBAKA RAFIKI WA KIKE WA KIJANA WAKE AFUNGWA MIAKA 35 JELA...

Mahakama ambako hukumu hiyo ilitolewa.
Baba mwenye umri wa miaka 67 amehukumiwa kifungo cha miaka 35 jela baada ya kumbaka rafiki wa kike wa kijana wake pale alipojihifadhi nyumbani hapo baada ya dansi.

Ismael Cruz, alipatikana na hatia na mahakama mwezi uliopita ya kumshambulia msichana wa miaka 19 akiwa amelala nyumbani kwa baba huyo huko San Antonio, Mei 2012.
Binti huyo aliieleza polisi aliamka na kukuta amevuliwa nguo nusu na kwamba Cruz alikuwa amejilaza juu yake.
Pale alipogundua mtu aliyembaka alikuwa baba wa rafiki yake wa kiume, mwathirika huyo alipiga kelele za kuomba msaada, kwa mujibu wa gazeti la San Antonio Express News.
Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, kijana wa Cruz alimpiga, na kuendelea kujaribu kumshambulia baba yake baada ya polisi kuwasili.
Cruz, ambaye alifungwa jela mara mbili kabla kwa kuendesha gari huku akiwa amelewa pombe, alisema alikunywa bia zaidi ya 60 usiku huo aliofanya ubakaji.
Mwanasheria wake alimwomba jaji kumfunga miaka 25 jela lakini akamhukumu kifungo cha miaka 35.

No comments: