MCHUNGAJI AKAMATWA AKIKARIBIA KUCHOMA MOTO VITABU 2,998 VYA KORAN...

KUSHOTO: Mchungaji Terry Jones akiingizwa kwenye gari mara baada ya kukamatwa. KULIA: Mchungaji Terry Jones.
Mchungaji Terry Jones amekamatwa jana wakati akielekea kuchukua vitabu vya Koran tukufu vilivyomwagiwa mafuta ya taa kwenda kwenye bustani, ambako mchungaji huyo amesema alikuwa amepanga kuchoma vitabu hivyo 2,998 - kimoja kwa kila mwathirika wa mashambulio ya kigaidi ya Septemba 11.

Polisi huko Polk County, Florida, walimkamata Mchungaji Terry Jones, mwenye umri wa miaka 61, na mchungaji mshirika wake, Marvin Sapp Jr, mwenye umri wa miaka 44, kila mmoja kwa shitaka la jinai la uchukuzi wa mafuta kinyume cha sheria.
Jones alisema alikuwa akielekea kwenye hifadhi moja ya jirani huko Mulberry kuchoma vitabu hivyo vya Koran jana Jumatano, Maadhimisho ya 12 ya mashambulio hayo. Maofisa walisema kwamba Jones pia alishitakiwa kwa kubeba hadharani kinyume cha sheria silaha ya moto, kosa dogo, na kwamba Sapp anakabiliwa na shitaka la kutokuwa na leseni hai ya gari hilo.
Wote waliwekwa mahabusu jana usiku kwenye gereza la Polk County, kwa mujibu wa Mkuu wa Usalama Grady Judd.
Meya wa Mulberry, sambamba na maofisa waliochaguliwa katika eneo hilo, msaidizi wa mkuu wa usalama na wakazi kadha wa Polk County wamezungumzia umuhimu wa kuonesha upendo na uvumilivu kwa imani zote Septemba 11.
Jones ni mchungaji wa kanisa dogo la kiprotestanti la Kikristo. Alianza kufahamika kwa mara ya kwanza mwaka 2010 pale alipopanga kuchoma Kuran wakati wa maadhimisho ya Septemba 11, japo alidhibitiwa kabla ya kufanya uhalifu huo.
Wafuasi wake walichoma kitabu hicho takatifu cha Kiislamu mnamo Machi 2011 na mwaka jana alizindua filamu ya kupinga Uislamu. Matukio yote matatu yaliibua ghasia huko Mashariki ya Kati na Afghanistan.
Ghasi zote zilitokea baada ya kuchomwa moto Koran mwaka 2011 huku waandamanaji wakivamia jengo la Umoja wa Mataifa mjini Mazar-i-Sharif huko kaskazini mwa Afghanistan, na kuua watu 7 wa mataifa mengine, wakiwamo walinzi wanne raia wa Nepal.
Jone mara kadhaa amekuwa akipuuza wito kutoka kwa jeshi la Marekani uliomtaka kutofanya maandamano yake. Maofisa wa jeshi wamesema maamuzi yake yameviweka vikosi vya Marekani na Magharibi nchini Afghanistan na kwingineko katika hatari.
Mulberry ni mji wenye wakazi takribani 3,000 kati ya Orlando na Tampa na hauna mahusiano yoyote na kanisa la Jones, ambalo hivi karibuni liliondoka kwenye jengo lake la Gainesville.
Mahakama ya Misri ilimtia hatiani Jones, sambamba na Wakristo saba wa Kanisa la Misri, bila kuwapo mahakamani, likiwahukumu kifo kwa mashitaka yaliyohusishwa na filamu hiyo. Hukumu hiyo ilionekana kwa kiasi kikubwa kama ishara sababu Jones na washitakiwa wengine wanaishi nje ya Misri.

No comments: