MWENZAKE NA LWAKATARE KESI YA SUMU AENDELEA KUSOTA RUMANDE...
Mshitakiwa Ludovick Joseph anayekabiliwa na kesi ya kula njama ya kudhuru kwa sumu, pamoja na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare, ameendelea kusota rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Juni 11 mwaka huu, Lwakatare aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kusaini hati ya Sh milioni 10 na kuwa na wadhamini wawili waliosaini hati ya Sh milioni 10 na kuwasilisha hati yake ya kusafiria.
Jana kesi hiyo ilitajwa mbele ya Hakimu Aloyce Katemana ambaye aliiahirisha hadi Julai 22 mwaka huu, baada ya Joseph kushindwa kutimiza masharti hayo na kurudishwa rumande.
Awali, Lwakatare na Joseph, walikuwa wakikabiliwa na mashitaka ya ugaidi katika mahakama hiyo, mashitaka ambayo yalikuwa hayana dhamana. Mei 8 mwaka huu Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliwafutia mashitaka hayo na kubaki na shitaka hilo la jinai linalodhaminika.
Washitakiwa hao wanadaiwa Desemba 28 mwaka jana katika eneo la King’ongo Kimara Stop Over Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, walipanga njama ya kutenda kosa la jinai la kutumia sumu kumdhuru Mhariri wa gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.

Comments