![]() |
Jengo la Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA). |
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeutaka uongozi wa televisheni ya Star TV na kisumbuzi cha Star Times kufika bila kukosa katika kikao maalum cha kujitetea kitakachofanyika Jumatatu ijayo baina yao na mamlaka hiyo kujieleza ni kwa nini wasichukuliwe hatua kwa kusitisha matangazo na kukiuka agizo la kuyarejesha.
Aidha mamlaka hiyo imesema kwa kuwa wote wamekiuka sheria na kanuni za mawasiliano kwa kutomshirikisha mdhibiti (TCRA) katika tofauti zao tangu awali, kikao hicho kitahusisha kutoa maamuzi ya kile walichokifanya kinyume cha sheria na hatua zitachukuliwa kwa atakayekaidi kufika.
Agizo hilo, limetolewa kwa mara nyingine jana na TCRA kutokana na vyombo hivyo vya mawasiliano kukiuka agizo la mamlaka lililotolewa na Mkurugenzi Mkuu, Profesa John Nkoma, Jumatatu wiki hii la kurejeshwa matangazo ya Star TV kwenye kisumbuzi cha Star Times. Yaliyoondolewa saa sita usiku wa Juni 08 mwaka huu.
Akizungumza na mwandishi katika ofisi za mamlaka hiyo, Dar es Salaam, jana Kaimu Meneja Mawasiliano wa TCRA, Semu Mwakyanjala alisema mamlaka hiyo inafuatilia kwa karibu ukiukwaji wa agizo hilo la kurejesha mawasiliano mara moja na pia sababu za Star TV kujitoa Star Times hivyo inasisitiza wahusika kufika katika mkutano Jumatatu, Juni 17 bila kukosa.
“Si Star TV wala Star Times walio sahihi katika kile walichokifanya, wote wamekiuka sheria za mawasiliano kwa sababu ikiwa wangekuwa na kutokuelewana miongoni mwao, walipaswa kulileta suala lao kwa regulator (mdhibiti-TCRA), wamewakosea Watanzania na wamekiuka sheria na kanuni,” alisema Mwakyanjala.
Mwakyanjala alisema wakati hilo likifanyika, mamlaka inawahakikishia umma wa Watanzania kuwa inaendelea kusimamia sekta ya mawasiliano kwa mujibu wa sheria na itakapohitajika, sheria itachukua mkondo wake.
Usiku wa Juni 08 mwaka huu, Star TV ilisitisha matangazo yake kupitia Star Times na kwa mujibu wa barua zake, ilisema imefanya hivyo kwa matakwa yake. Pia juzi kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, ilitishia kwenda mahakamani kuishitaki TCRA kwa kuilazimisha kurejea Star Times.
Katika taarifa yake, Star TV inadai haina mkataba wa kisheria baina yake na Star Times wa kurusha maudhui yake nje ya nchi jambo linaloamini inakiuka sheria ya Hatimiliki. Pia inadai kisimbuzi hicho kinakiuka Sheria ya Mawasiliano ya Kielektronikia na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 na kanuni zake na TCRA kwa upande wake inasema vyombo hivyo pia vimekiuka sheria hiyo ya EPOCA na kanuni zake.

No comments:
Post a Comment