![]() |
| Mtambo wa kusafirishia gesi ulioko Mtwara. |
Vurugu zilizotokana na upotoshaji kwa wananchi kuhusu gesi asilia zilizotokea Mtwara na Masasi, zimesababisha baadhi ya wawekezaji kutishia kutoendelea kuwekeza katika mkoa huo, wakisuburi hali iwe shwari.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema alitoa kauli hiyo bungeni jana, wakati akitoa taarifa ya Serikali kuhusu namna suala la sakata la gesi asilia mkoani Mtwara lilivyoshuhulikia, kabla ya kuanza kujibu maswali ya papo kwa hapo bungeni Dodoma.
Alisema, mgogoro huo uliotokana na wanasiasa kupotosha na elimu kutowafikia wananchi kwa wakati, umechangia wawekezaji wengine kusubiri miezi mitatu hadi sita kabla ya kuendelea kuwekeza.
Alitoa mfano wa wawekezaji wanaotafuta gesi katika kina kirefu cha bahari, ambao alisema wametishia kutoendelea kutafuta gesi hadi hali iwe shwari katika maeneo hayo, jambo ambalo Serikali inaendelea kuliweka sawa.
Waziri Mkuu alisema, Serikali inaangalia namna ya kuwalipa fidia wale wote walioharibiwa, kuchomewa na kupoteza raslimali zao kutokana na vurugu za gesi asilia mkoani Mtwara na wilayani Masasi.
Aliwapa pole wale wote ambao kwa namna moja au nyingine wamepata hasara kutokana na vurugu hizo, ambazo aliomba zisiwe sababu ya kuwagawa Watanzania kutokana na matumizi ya raslimali.
Alisema raslimali ya gesi itawanufanisha wananchi wa Mtwara kwa kujengwa kiwanda cha kusindika gesi ghafi kabla ya kuisafirisha kwenda Dar es Salaam, ambako Serikali inatarajia kuokoa fedha
nyingi kuendesha mitambo na viwanda. Kwa sasa Serikali inatumia zaidi ya Sh trilioni 1.6 kununua dizeli kwa mwaka.
Waziri Mkuu aliwataka wananchi wote nchini wakiwamo viongozi wa vyama vya siasa, kuanza kuzungumza lugha moja ya umoja na amani kutokana na ukweli kwamba hali ya mvutano wa gesi imemalizika mkoani Mtwara.
Aliahidi kwamba Serikali itaendelea kutoa elimu na kuwasiliana na kuwashirikisha wadau mbalimbali na wananchi katika jambo lolote linalotokea, ili kuhakikisha kila jambo linakuwa wazi kwa wahusika.
Awali wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe, alitaka Serikali iwachukulie hatua wale wote ambao walishiriki katika vurugu hizo.
Lakini Waziri Mkuu alissema pamoja na kwamba wajibu wa kuwawajibisha anao Rais, lakini ni bora kusitafutwe mchawi.
Alisema kwa kiasi kikubwa vurugu za gesi asilia zimechangiwa na vyama vya siasa kutafuta maslahi ya kisiasa kwa malengo ya kupata mafanikio ya kisiasa katika maeneo hayo.
“Vyama vya siasa vilichangia vurugu hizo kutokana na kwenda na agenda za kisiasa kwa lengo la kutafuta ushindi wa kisiasa hapo baadaye na kusahau kwamba hali ikichafuka, hakuna atayakepata nafuu,” alisema.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, ambaye nyumba yake ilichomwa moto katika vurugu hizo, alisema amewasamehe wote na
anamwachia Mungu.
Alisema, Mungu ndiye aliyempa uwezo wa kujenga nyumba hiyo na katika mazingira hayo, hana la kusema anamwachia Mungu.
Baada ya kauli hiyo, kipindi cha maswali na majipo kilipomalizika, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alifuta uamuzi wa kuunda tume ndogo ya Bunge ya kwenda kuzungumza na wananchi wa Mtwara, kuhusu mgogoro huo.
Alisema Bunge limejiridhisha na taarifa ya Waziri Mkuu na kuona kwamba kuundwa kwa tume, itakuwa sawa na kurudia mambo yaliyokwishafanyika.
Makinda alisema kazi iliyobaki mbele ya wabunge ni kuona ahadi zilizotolewa na Serikali kupitia Waziri Mkuu, zinatekelezwa.
Katika kusimamia kazi hiyo, Makinda aliahidi wabunge kukutana na kuunda kamati zinazohusu ahadi hizo kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji.
“Nilikuwa nimeeleza kwamba tutakuwa na tume ndogo, napenda nichukue nafasi kueleza kwamba
tunamshukuru Waziri Mkuu na wananchi kwa kuwa wawazi kuzungumza na Waziri Mkuu. Sisi tumepata faida ya kujua nini kilikuwa tatizo,” alisema.
Spika aliomba Watanzania kujifunza kama yapo matizo makubwa na ujumbe wa Serikali ukaenda, watambue kwamba watapata majibu na kushukuru makundi mbalimbali yaliyokutana na Waziri Mkuu na kufikia maelewano.
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR Mageuzi), alihoji ni
namna gani wabunge wataweza kuona mikataba ya gesi akiomba Spika awapatie utaratibu
wa kufanikisha hilo.
Mkosamali ambaye aliomba mwongozi wa Spika, alijibiwa kwamba upo utaratibu wa muda mrefu wa kumwezesha mbunge kuona na kusoma mikataba hiyo.
Alisema ofisi ya Katibu wa Bunge ndiyo inayoshughulika na suala hilo kwa kumtaka mbunge aandike barua kwenda ofisi hiyo.
“Watakupa mkataba huo utasoma kwa matumizi yanayohusika,” alisema Spika Makinda.

No comments:
Post a Comment