Rubani mmoja kauchapa usingizi mzito wakati akiongoza ndege ya abiria iliyokuwa maelfu ya futi juu angani.
Rubani wake msaidizi alikuwa ameruhusiwa kwenda kujisaidia msalani na ndipo aliporejea na kujaribu kuomba kufunguliwa mlango wa chumba cha marubani kwa kutumia simu ya mawasiliano ya ndani, lakini ilikuwa ikiita tu bila majibu.
Kisha baadaye alipoweza kuingia kwenye chumba cha marubani baada ya juhudi kubwa, alipatwa na mshituko kukuta mwenzake akiwa amelala fofofo.
Uchunguzi umeanza kufanywa na shirika la ndege la Uholanzi la Transavia kujua nini hasa kilichotokea katika ndege aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikielekea Crete.
Ingawa tulio hilo lilitokea Septemba mwaka jana, ilifahamika hadharani juzi kutoka kwa Bodi ya Usalama ya Uholanzi (OVV) katika ripoti iliyochapishwa kwenye tovuti yake.
Bodi hiyo imeliita tukio hilo kuwa 'la hatari'.
"Baada ya masaa mawili na nusu angani, rubani wa ndege hiyo iliyosajiliwa nchini Uholanzi alitoka kwenye chumba chake na kwenda msalani," OVV ilisema.
"Muda mfupi baadaye alitaka kurejea kwenye chumba cha marubani. Alipotumia simu ya ndani kuwasiliana na ofisa wa kwanza amfungulie mlango hakupata majibu yoyote, akamkuta ofisa huyo akiwa amelala usingizi mzito."
Septemba makundi ya marubani yalitahadharisha kwamba masaa mapya ya kuruka na ndege angani yaliyowekwa na Umoja wa Ulaya yanaweza kusababisha matatizo makubwa.
Chini ya sheria hizo mpya, marubani wanaweza kushusha ndege za kibiashara baada ya masaa 22 - ikiwamo masaa 11 ya kuruka angani, pamoja na muda wa kusubiria na kwenda uwanja wa ndege.
Wabunge walionywa kwenye ripoti yao ya awali kwamba masaa 22 ya kufanya kazi mfululizo ilikuwa "kitu kigeni' - hasa kwa urukaji wa usiku - kwamba unaongeza kiwango cha uchovu kulingana na kile cha 'ulevi.'
Marubani wa Uingereza kwa sasa wanaruka masaa hadi masaa 18 bila kulala - lakini zaidi ya marubani wanne kati ya kumi tayari wameripotiwa kulala wakiwa angani - ambapo wa tatu anapoamka na kukuta rubani mwanzake pia amelala.
Sheria mpya zinatarajiwa kuingizwa kwenye sheria za Umoja wa Ulaya baada ya nusu ya mwaka 2013 na kuanza kutumika rasmi mwishoni mwa 2015.

No comments:
Post a Comment