Wavutaji sigara wakorofi wamelazimisha ndege ya Sunwing iliyokuwa safarini kutoka Halifax kwenye Jamhuri ya Domonika kutua Bermuda Ijumaa.
Mara tu walipotua Bermuda, polisi waliingia ndani ya ndege na kuwakamata abiria watatu.
"Inaonekana kuwa ni baba, mama na mtoto. Wazazi hao wanaonekana kuwa na umri wa takribani miaka 50. Mtoto, naamini, yuko katika miaka kama 22 hivi," Kaimu Inspekta Paul Simons alisema kwa huzuni.
Familia hiyo imeamriwa kubaki Bermuda na pasi zao za kusafiria na nyaraka za safari zimeshikiliwa na mamlaka husika.
Abiria waliosumbuliwa na kubadilika kwa ratiba hiyo walipatiwa vyumba kwenye hoteli na kupakiwa kwenye ndege nyingine siku ya Jumamosi.
Inaonesha kuna baadhi ya watu hawajali ilani za kutovuta sigara kwenye ndege na ukweli kwamba unatakiwa kusikiliza maelekezo ya wafanyakazi wa ndege," ilisema moja ya taarifa zilizotumwa kwenye mtandao wa airliners.net, 'tovuti kubwa na inayotembelewa na wengi inayoelimisha kuhusu mambo ya usafiri wa anga kwenye intaneti.'
Kwa huzuni, hii hautakuwa usumbufu wa mwisho kwa abiria wa Sunwing.
Mgomo unatarajiwa kuanza hivi karibuni, ilisema CUPE, chama kinachowakilisha wahudumu 900 wa shirika hilo la ndege.
"Machi 2, siku sitini baada ya kuanza kwa kipindi cha majadiliano, chama cha wahudumu wa ndege hizo kitakuwa na haki ya kugoma," iliandika CUPE. "Wakati huo, kipindi cha majadiliano kinaweza kurefushwa kwa ridhaa ya pande zote mbili. Lakini kufuatana na mambo yalivyo sasa, chama hicho kina mashaka kwamba kinaweza kuafiki urefushwaji huo."
Chama cha wahudumu wa ndege za Sunwing kinajadiliana makubaliano yake ya kwanza kwa ujumla.

No comments:
Post a Comment