![]() |
| Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa kwenye harakati za kunusuru bidhaa zao baada ya moto kulipuka kwenye moja ya maduka Mwenge, Dar es Salaam jana. |
Moto mkubwa uliozuka jana umetekeeza kabisa maduka mawili ya vipodozi
katika eneo la Kituo cha Mabasi cha Mwenge jijini Dar es Salaam, ingawa
hakuna madhara kwa maisha ya watu.
Moto huo uliowaka kwa takribani nusu saa ulizuka ghafla kwenye moja ya maduka katika eneo lenye maduka 14 na kuenea duka jingine kabla ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji cha Jiji kufika kusadiaia juhudu za wananchi katika kuzima moto huo.
Kabla ya kufika kwa kikosi hicho, baadhi ya wamiliki wa maduka jirani walikubwa na taharuki na kuonekana wakihaha kuokoa mali zao kwenye maduka huku baadhi wakionekana kuzima moto kwa kutumia ndoo na mipira ya maji.
Baadhi ya watu akiwamo mmiliki wa mgahawa wa Mwenge Complex walilazimika kupanda juu ya paa na kutumia maji aliyohifadhi kwenye mataki na kuyatumia katika kuzima moto huo.
Mmoja wa mashuhuda wa moto huo aliyejitambulisha kwa jina moja ya Yusuf alisema kuwa moto huo ulianzia kwenye duka moja linalofanya kazi za kuchomelea baada ya nyanya kulipuka kutokana na umeme mdogo.
Hata hivyo, polisi kutoka kituo cha Mwenge na baadhi ya wafanyabiashara walifanya kazi ya ziada ya kudhibiti vibaka wasiibe mali zilizokuwa zikitolewa kwenye maduka mengine ambao walikuwa na mashaka moto kusambaa zaidi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alithibitisha kutekeea kwa maduka hayo na kuwa thamani ya mali na chanzo cha moto bado havijajulikana na kuwa polisi inafanya uchunguzi wa kina wa janga hilo.
“ Kusema kweli wafanyabiashara wamepata hasara, mbali ya mali zilizoteketea kwa moto, lakini pia hata wale waliokuwa na kazi ya kuokoa mali zao zingine zimeharibika na maji na nyingine kutokana na uwekaji wa bidhaa hizo,” alisema.
Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida na watu kutojua mbinu za kujihami panapokuwa na majanga, wakati moto huo ukiendelea kupamba moto, baadhi ya mabasi ya abiri yalikuwa ndani ya kituo hicho badala ya kuyaondoa ili kuepusha hatari na madhara zaidi.

No comments:
Post a Comment