![]() |
| Kichanga hicho kikiwa chini ya uangalizi maalumu. |
Msichana wa miaka tisa amejifungua mtoto wake mwenyewe,
mamlaka za nchini Mexico zimebainisha jana.
Kichanga hicho cha kike kilizaliwa Januari 27 katika
Hospitali ya Zoquipan, mjini Zapopan, kwenye jimbo la Jalisco lililoko
magharibi mwa Mexico. Alizaliwa akiwa na uzito wa kilo 2.7.
Mama wa msichana huyo, aliyefahamika kwa jina moja la Dafne,
aliwaeleza maofisa wa polisi: "Msichana huyo walikuwa amezidi kidogo miaka
minane ndipo alipopata ujauzito. Baba wa kichanga hicho ni mvulana ambaye ana
miaka 17, lakini hatujamuona, tangu alipotoweka kusikojulikana."
Jorge Villasenor kutoka ofisi ya waendesha mashitaka wa
serikali, alisema: "Tunamsaka kijana huyo kupata taarifa zake sababu
msichana hafahamu chochote kilichotokea.
"Hii ni kesi ya ubakaji au udhalilishaji watoto
kijinsia."
Wasichana wote hao wameruhusiwa kutoka hospitali mwishoni
mwa wiki iliyopita, kwa sasa wanaendelea vema lakini hospitali hiyo ilisema
italazimika kufanya ufuatiliaji wa karibu na wa mara kwa mara kufuatia umri
mdogo wa mama huyo mpya.
MAMA WENYE UMRI MDOGO ZAIDI DUNIANI:
1. Lina Medina, kutoka Ticrapo nchini Peru, alijifungua
mtoto wa kiume aliyemwita Gerardo kwa upasuaji akiwa na miaka mitano na miezi
saba Mei, 1939. Wazazi wake walidhani alikuwa na uvimbe lakini alipopelekwa
hospitali, akagundulika kuwa na ujauzito wa miezi saba.
2. Yelizaveta "Liza" Gryshchenko, ndio alikuwa
ametimiza tu miaka sita wakati akijifungua mtoto njiti wa kike nchini Urusi
Agosti, 1934. Baba wa kichanga hicho alikuwa ni baba mzazi wa Liza aliyekuwa na
miaka 69. Familia hiyo ihama baada ya kashfa hiyo.
3. Msichana wa miaka sita, aliyefahamika kama 'H'
alijifungua kichanga cha kike kwa upasuaji Juni, 1972 mjini Delhi, India.
Mwanzoni alilazwa hospitali kwa kile kilichodhaniwa kuwa ni uvimbe usio wa
kawaida.
4. Msichana wa India ambaye hakufahamika alifariki wakati
akijifungua, sambamba na kichanga chake Agosti 1933. Alikuwa na miaka minane
tu.
5. Griseldina Acuna kutoka Colombia, aliripotiwa kuwa
alianza kupata hedhi akiwa na miaka mitatu na kujifungua kichanga cha kiume
Septemba, 1936, akiwa na umri wa miaka minane na miezi miwili. Baba wa kichanga
hicho anadhaniwa kuwa ni mmoja wa marafiki wa familia hiyo.

No comments:
Post a Comment