Madaktari wa Kim Kardashian wanadhani mtoto wake aliye
tumboni anaweza kuwa katika hatari sababu ya mawazo yanayosababishwa na Kris
Humphries kuchelewesha talaka yao … imefahamika.
Vyanzo vya habari vinavyofuatilia suala hilo kwa ukaribu
vimesema … siku kadhaa zilizopita Kim alimwita daktari wake katikati ya usiku
kwenda nyumbani kwake sababu alikuwa akisikia maumivu makali. Daktari huyo
alimchunguza, lakini baadaye akaonya anaamini matatizo hayo kwa kiasi kikubwa
yanatokana na mawazo.
Vyanzo vimesema … mawazo pekee kwa sasa katika maisha yake
ni talaka. Na Jumanne masaa kadhaa kabla ya kukutana na mwanasheria wake,
disso-queen Laura Wasser, maumivu ya Kim yalirejea tena kwa kishindo.
Madaktari wamemuonya Kim anahitaji kukabiliana na mawazo au
vinginevyo kunaweza kuwa na 'athari za muda mrefu.' Daktari huyo hakufafanua,
lakini imeelezwa mhemuko wa Kim kwa mtoto wake huyo mpya unaweza kumuweka
hatarini.
Mama wa Kim, Kris Jenner akiwa katika kipindi
cha "The View" jana, alisema, "Kim amekuwa akishughulikia suala
lake hili la talaka kwa miezi. Amekuwa katika shinikizo kubwa sababu ya jambo
hili na madaktari walimweleza amekuwa na wiki ngumu mno na mawazo yanaweza kuja
kuwa tatizo endapo hatokuwa makini.
No comments:
Post a Comment