![]() |
| KUSHOTO: Cheryl Maddison. KULIA: Mohamed Fadel el Anssari wakati akisikiliza kesi yake. |
Mhudumu wa hoteli amefungwa miaka 23 jela kwa kubaka na
kujaribu kumuua mwanamitindo wa Uingereza kwenye hoteli moja maarufu.
Raia wa Morocco, Mohamed Fadel el Anssari mwenye miaka 31,
alipatikana na hatia ya kumbaka Cheryl Maddison kabla ya kujaribu kumnyonga,
akimchoma visu mara kadhaa na kumtelekeza akisubiria kifo baada ya kurejea
kazini akitoka kazini kwenye hoteli ya Magaluf, mjini Majorca, mwaka 2008.
Alinusurika katika mateso hayo tu pale alipojifanya kuwa
amekufa ili kujiepusha na majeraha zaidi.
El Anssari alihukumiwa miaka 11 kwa shambulio la ubakaji
dhidi ya Cheryl na miaka mingine 12 kwa kujaribu kumuua mwanamke huyo.
Majaji walisema kwamba shambulio hilo lilifanyika katika
mazingira ya 'vurugu na vitisho.'
Hukumu yao ilitangazwa katika waraka wenye kurasa 52
uliotolewa hadharani mchana.
Cheryl, sasa miaka 25, ambaye hapo kabla alificha
utambulisho wake ili kuweza kuzungumzia shambulio hilo, alimwaga machozi baada
ya kuelezwa habari hizi akiwa nyumbani kwake huko Houghton Le Spring, mjini Country
Durham.
Uhalifu wa El Anssari ulielezewa na majaji kama 'mbaya mno'
kiasi kwamba wangeweza kuhakikisha wanatoa kifungo cha muda mrefu jela.
Cheryl alishambuliwa majira ya Saa 1 alfajiri ya Mei 30,
2008 wakati akiwa njia kwenda nyumbani baada ya kumaliza zamu yake kazini
katika baa.
Alichomwa visu mara kadhaa kwenye shingo, kooni na mgongoni
baada ya Anssari kuwa ameingia kwa nguvu kwenye makazi yake anayoishi na
kumbaka.
Mahakama ilielezwa jinsi alivyomchoma visu kifuani kwake
huku akiwa amelala hajitambui kufuatia shambulio la ubakaji na kisha
kumlazimisha kusimama baada ya kumzunguka na kumchoma kisu shingoni mwake.
Cheryl, ambaye amehamia Majorca siku sita tu kabla ya
shambulio hilo, alijifanya kuwa amekufa hadi Anssari alipotokomea kabla kuinuka
na kutimkia mitaani kuomba msaada na kuanguka kwenye dimbwi la damu.
Alitumia wiki mbili akiwa amelazwa hospitali baada ya hapo
huku madaktari wakisema alikuwa mwenye bahati kunusurika kifo.
Mahakama hiyo ilielezwa jinsi jirani, Laura Pamela,
alivyosikia kelele za Cheryl lakini akazipuuzia akidhani kuwa 'ni ugomvi
mwingine' uliohusisha wanandoa wa Uingereza.
Anssari alikamatwa Julai, 2011 kufuatia msako mkali wa
polisi uliochukua muda mrefu.
Wapelelezi waligundua sigara aliyodondosha
mtaani na kukuta inafanana na vipimo vyake vya DNA ambavyo vilikutwa kwenye
eneo la tukio la uhalifu huo.
No comments:
Post a Comment