Familia ya mwanajeshi aliyeuawa katika Vita ya Kwanza ya Dunia imeunganishwa tena kupitia medali yake ya ushindi - baada ya medali hiyo kuokotwa kwenye mfereji wa maji machafu.
Askari asiye na cheo, Charles William Curtin aliuawa huko Ypes Mei mwaka 1915, akiwa na umri wa miaka 35 tu, na tuzo hiyo baada ya kufa kwa ajili ya ujasiri wake nchini Ufaransa ilikabidhiwa kwa familia yake changa aliyoiacha.
Lakini medali hiyo ya shaba ilipotea na haikuweza kupatikana kwa zaidi ya miaka 70.
Sasa kitu hicho kilichorithiwa vizazi kwa vizazi kimerejeshwa kwa wajukuu wa Curtin, John Hodgson na Dorothy Heed, baada ya kuwa imepatikana kwenye mfereji wa maji machafu huko Manchester kwa msaada wa kibarua.
Shemeji wa kibarua huyo, mhasimu mstaafu Christine Wolstenholme, alitumia miaka mitatu kuitafuta familia hiyo hivyo kuweza kurejesha hazina hiyo kwenye mikono sahihi.
Mafanikio ya mtu huyo mwenye miaka 66 yamekuwa ya kuvutia sababu medali hiyo ilikuwa imechongwa maandishi ikiwa na makosa kidogo kwenye jina.
Hodgson kutoka Poulton, karibu na Blackpool alisema: "Simu iliita siku moja na mwanamke akauliza kama nilikuwa John Hodgson na kama nilikuwa na ndugu huko Chorlton anayeitwa Curtin.
"Alisema mwanafamilia wake mmoja alikuwa akisafisha mitaro mjini Manchester na akaokota medali na kwamba alikuwa ametumia miaka kadhaa tangu aanze kutafuta mmiliki halali wa medali hiyo.
"Hakika nilistaajabu mno kwakweli. Hasa kutokana na binamu yangu Anne kujaribu kutafuta medali ilikokwenda. Ukweli alitumia muda wote huu kufanya utafiti kwa wageni ni inashangaza mno."
Mtu huyo mwenye miaka 70 - ambaye hakuwahi kuiona medali hiyo - alisema hakuwahi kujua kiundani kuhusu babu yake.
Curtin aliajiriwa kwenye batalioni ya pili, Royal Lancaster Regiment, akiwa na umri wa miaka 16 tu.
Alimuoa Anne Shelmerdine mwaka 1909 wakati akiwa na miaka 26 na waliishi huko Chorlton-on-Medlock, mjini Manchester.
Baada ya Vita ya Kwanza ya Dunia kuanza, alipelekwa Ypres, na hakuweza kurudi kwa mke wake na watoto.
Kumbukumbu zilionesha kwamba aliuawa katika mapambano Jumamosi ya Mei 1, 1915, katika shambulio la pili la Ypres, ambalo lilisababisha vifo vya watu 100,000.
Wawili hao walifanikiwa kupata mabinti wawili - Alice, ambaye alifariki utotoni na Mama wa Hodgson Annie, ambaye alikuwa na miaka miwili tu wakati baba yake alipouawa.
Tangazo la kifo lililoandikwa na Anne lilichapwa kwenye gazeti la Manchester Evening News. Lilisomeka: "Kila mara tunatulia na kukufikiria na kuwaza jinsi ulivyokufa. Kufikiri hukuweza kusema kwaheri kabla hujafumba macho yako. Kwa huzuni unakumbukwa na mkeo na familia."
Anne aliolewa tena baada ya vita ya mwaka 1923, na yeye na mumewe mpya William Dewhurst walifanikiwa kupata mtoto waliyemwita Wilfred. Anne alifariki mwaka 1940 akiwa na miaka 60.
Hodgson, mhandisi mstaafu wa televisheni, alisema: "Ninazo picha za zamani za baba yangu kabla hajakwenda vitani -kitu fulani ambacho askari wote wangeweza kufanya endapo wasingerejea tena. Napendekezeka ifanyike pia kwa wanajeshi wa leo.
"Kitu cha kuhuzunisha ni kwamba hakuwahi kumwona mama yangu akikua, watoto hao hawakuwa na baba, na kumekuwa na makumi elfu ya watoto leo hawakui na baba zao sababu ya vita."
Medali hiyo ya njano ya shaba inaweza hapo awali kuwa ilining'inizwa kwenye utepe wenye rangi za upinde wa mvua na ilitunukiwa kwa wote ambao walitumikia Vikosi vya Jeshi katika wakati wa vita.
Hodgson alisema: "Hainoneshi kuhamasisha kwa sasa - imepuuzwa kwa kiasi fulani na kufifiishwa - lakini ina thamani kihistoria na kimaono.
"Inashangaza mno kuipata tena - haikutarajiwa kabisa. Mwanamke huyo alikuwa na amani mno kwa ameipata familia husika.
"Swali lililobakia ni kwamba, iliingiaje kwenye mtaro wa maji machafu? Nasema kwamba hatuwezi kufahamu."
Medali hiyo, yenye maneno: 'The Great War for Civilisation' (Yaani 'Vita Kuu kwa Ustaarabu'), ilikutwa ikiwa imetupwa katika mtaro wa maji machafu mjini Chorlton mwaka 2007 na shemeji wa Christine.
Medali hiyo ilikuwa na rejimenti na namba kwenye pande zake lakini ilikuwa imechongwa maandishi yenye jina la 'Pte C Williams', wakati jina la askari huyo lilikuwa Charles William Curtin.
Kibarua huyo hajafanya chochote kuhusu ugunduzi wake huo kwa miaka miwili, pale alipokabidhi kwa jamaa zake begi la vitu vilivyopotea alilookota. Aliamua kufanya mpango wake wa kuisaka familia ya ndugu wa mtukuniwa huyo wa medali hiyo.
Christine mwenye miaka 66, kutoka Wem, karibu na Shrewsbury, huko Shropshire, alisema: "Nilifahamu itakuwa ni sawa na kutafuta sindano kwenye msitu mnene, lakini nilikuwa nimedhamiria kujua familia gani inayohusika na medali hiyo na lilikuwa jambo sahihi kufanya.
"Ilikuwa ni kazi kubwa lakini yenye thamani kubwa na nimefarijika mno medali imerejea kwa wamiliki wake sahihi."
Mpango huo uliingia dosari pale alipougua, lakini akaendelea tena na mpango wake mwaka jana.

No comments:
Post a Comment