KANUNI ZA BUNGE 'ZAMVUA KITANZI' JAMES MBATIA...
Taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka bungeni mjini Dodoma ni kwamba, Mbunge wa Kuteuliwa James Mbatia sasa anaweza kulala usingizi mzuri baada ya 'kunasuliwa kitanzi' na kanuni za bunge.
Katika kikao cha Bunge kinachoendelea asubuhi hii, Mwenyekiti Jennister Mhagama, alitolea ufafanuzi kuhusu kauli aliyoitoa Mbatia siku chache zilizopita kwamba endapo serikali ingewasilisha bungeni humo mitaala ya elimu, basi yeye angejiuzulu ubunge.
Ufafanuzi huo ulitolewa kufuatia hoja ya Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangala kutaka Bunge limshinikize Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, kutekeleza uamuzi wake wa kujizulu ama sivyo Bunge limsimamishe ubunge.
Hoja hiyo ilizusha malumbano kwa dakika kadhaa baada ya Mbunge mwingine wa NCCR-Mageuzi, Moses Machalli kupinga vikali na ndipo Mwenyekiti akalazimika kuingilia kati.
Katika maamuzi yake, Mwenyekiti Mhagama alitoa kauli ambayo inaweza kuwa faraja kubwa kwa Mbatia kufuatia shinikizo lililokuwa likimzonga kwa siku kadhaa sasa la kutakiwa kutimiza kauli yake.
Katika maamuzi hayo, Mhagama alisema kwamba Bunge linaongozwa na kanuni, hivyo kwa kufuata kanuni hizo hakuna kipengele chochote kinachoweza kumshinikiza Mbatia kujiuzulu
Aliongeza kuwa uamuzi wa kujiuzulu uko mikononi mwa Mbunge huyo baada ya kupima uzito wa suala hilo kama unamlazimu kufanya hivyo.
Kwa kuangalia mwa mapana na marefu, blogu hii haioni uwezekano wowote wa Mbatia kujiuzulu ubunge hasa kutokana na ukweli kwamba nafasi hiyo ni 'lulu' kwake na chama chake.

Comments