Friday, February 8, 2013

CHEKA TARATIBU...


Mama mmoja wa Kichagga kaenda kwa mara ya kwanza kwenye hoteli moja ya kitalii. Akaketi meza moja na wazungu watatu. Mara mhudumu akaja na kuwauliza wale wazungu kinywaji watakachokunywa. Wa kwanza akazema, "JOHN WALKER SINGLE". Wa pili akasema, "CAPTAIN MORGAN SINGLE". Wa tatu akasema, "JACKIE DANIEL SINGLE". Mama yule kwa ugeni wake akadhani walikuwa wakitaja majina yao na hali zao za mahusiano. Mhudumu alipomuuliza yule mama akajibu, "MANKA PANTASARI MUSHI MARRIED!" Kasheshe…

No comments: