![]() |
| Gaidi Osama bin Laden (kulia) na watoto wa moja ya shule za msingi Uttar Pradesh, India. |
Unapoomba kazi kwa kutumia majina feki, ni muhimu kuhakikisha kwamba, angalau kidogo, una ufahamu wa mambo kadhaa.
Hivyo pale gaidi aliyekufa 'Osama bin Laden' alipojibu tangazo la nafasi ya kufundisha kwenye Shule la Msingi nchini India mwaka jana, akimtaja Bill Clinton kama baba yake, haikuchukua muda mrefu kwa walimu kubaini kujizingizia kwake.
Alikuwa ni mmoja kati ya mamia ya majina ya vioja ya uongo ambayo wamekuwa wakijibatiza waombaji kwa matumaini ya kupata kazi kwenye shule mjini Uttar Pradesh, kaskazini mwa India.
Pengine kwa fikra za kutumiwa herufi za 'Abcdefgh' anaweza kuwa kwenye nafasi nzuri ya kufundisha watoto Kiingereza pale alipoieleza Wizara ya Elimu ya India kwamba jina la baba yake ilikuwa Xyz.
Au pengine Mungu wa Kihindu Jai Sri Ram alidhani anahitaji mapumziko kutokana na kazi za peponi kusaidia kusukuma matokeo ya elimu ya dini ya taifa hilo.
Kulikuwa pia na mwombaji mmoja ambaye alijipa jina la Farji, ambalo tafsiri yake ni 'feki'. Jina la baba yake liliandikwa Farji Singh.
Na katika hali ya kutoshangaza, waombaji hawa wote walikuwa na rekodi za aina yake kielimu, wakiwa wamepata alama asilimia 100 katika mitihani yao yote.
Wakati gaidi aliyekufa 'Osama bin Laden' alipoomba nafasi ya kufundisha katika shule moja ya msingi India mwaka jana, akimtaja Bill Clinton kama baba yake, haikuchukua muda mrefu kumbaini uongo wake.
Lakini badala ya kuyatupilia mbali maombi yao hayo, idara ya elimu ya msingi ya nchini humo ikawapatia wote namba za usajili na pia kuwapatia barua za ushauri kwa kutumia anwani zao 'feki'.
Waombaji wa aina hiyo, waliorodheshwa kwenye orodha ya kwanza ya waombaji kwa ajili ya kazi ya ualimu, wamefanya zoezi la kuajiri la Idara ya Elimu nchini humi kuwa kichekesho.
Waombaji hao ni wazi wamedanganya kila taarifa, kuanzia majina na anwani hadi kumbukumbu zao za mitahani.
Katika namna ya ajabu, uchunguzi wa maombi yaliyowekwa katika mtandao, umegundua zaidi ya asilimia 60 ya waombaji kuwa ni 'feki'.
Katika nafasi za kazi 72,825 za walimu wa shule za msingi, zaidi ya maombi laki 70 yalipokelewa kati ya hayo takribani 20 yanaaminika kuwa ni halisi.
Waziri wa nchi anayeshughulikia elimu ya msingi, Waseem Ahmad alisema idara hiyo itarekebisha makosa hayo.
"Huu utaratibu wa kupokea maombi kwa njia ya mtandao na kuyachambua kwa kutumia programu ya kompyuta ulikuwa na lengo la kuweka uwazi kamili.
"Inawezekana kuna matatizo fulani lakini yatapatiwa ufumbuzi katika siku zijazo," alinukuliwa akisema.
Katika namna ya kuvutia, wengi wa waombaji wamedai kupata alama zinazofanana za zaidi ya asilimia 95 katika mitihani yao yote.
Mfanyakazi wa ngazi za juu katika idara hiyo alisema: "Tatizo ni kwamba waombaji feki pekee wanaweza kuitwa kwa ajili ya usaili wa kwanza na wa pili sababu jumla ya alama zao zinaonesha kuwa kati ya asilimia 95 na 100."
Tangu nafasi za walimu wa shule za msingi kutangazwa kote kwenye eneo hilo, maelfu ya waombaji kutoka zaidi ya wilaya 20 wametuma maombi kwa matumaini watachaguliwa kwa ajili ya nafasi hizo.

No comments:
Post a Comment