![]() |
| Ndege ya Alaska Airlines. |
Ndege iliyokuwa ikielekea mjini Seattle ililazimika kutua kwa dharura baada ya nahodha wake kupoteza fahamu na hivyo kulazimisha nahodha msaidizi kubeba jukumu la kuiongoza ndege hiyo kutua kwa usalama.
Rubani wa Alaska Airlines alizimia ghafla akiendesha ndege angani na akalazimika kupatiwa matibabu na daktari humo humo kwenye ndege hiyo, ambayo ilikuwa imebeba watu 121.
Tukio hilo la juzi, ni mara ya pili mwaka huu kwamba rubani wa Alaska Airlines amepoteza fahamu ndani ya chumba cha marubani cha moja ya ndege za shirika hilo.
Januari 22, rubani msaidizi kwenye ndege ya Alaska Airlines iliyokuwa ikitokea Seattle kwenda Las Vegas alianguka na kupoteza fahamu kwa kipindi kifupi na kutakiwa kupatiwa matibabu.
Ndege hiyo, ambayo ilikuwa imebeba abiria 146, ilitua salama kwenye uwanja wa Las Vegas. Matukio hayo mawili hayafikiriwi kuhusiana, ABC News inaripoti.
Msemaji wa Alaska Airlines alisema kwamba katika tukio la juzi, rubani msaidizi alitoa taarifa ya kuwapo dharura ili aweze kupewa uangalizi wa upendeleo kwa rubani huyo baada ya kuwa amepoteza fahamu.
Rubani huyo, ambaye alirejewa na fahamu zake, alihudumiwa na daktari ndani ya ndege kabla ya kupelekwa hospitalini mara tu ndege hiyo ilipogusa ardhi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Portland.
Hakutajwa jina lake lakini ameripotiwa kuwa ameshafanya kazi katika shirika hilo kwa karibu miaka 30. Rubani msaidi ambaye aliiongoza ndege hiyo kutua salama amefahamika kufanya kazi katika shirika hilo kwa miaka 11.
Ndege hiyo aina ya Boeing 737-700 ilikuwa imebeba abiria 116 na wafanyakazi watano wakati iliporuka mjini Los Angeles majira ya Saa 12:30 jioni (Saa za Marekani) kuelekea upande wa kaskazini wa Seattle ambako ilitarajiwa kutua Saa 3:30 usiku (Saa za Marekani).
Badala yake ndege hiyo ilitua mjini Portland masaa mawili na nusu baadaye kufuatia rubani huyo kupoteza fahamu.
Abiria kadhaa walihamishiwa kwenye ndege nyingine kuelekea Seattle, wakati waliobakia walichukuliwa na ndege iliyopangwa kutua kwenye mji huo majira ya Saa 1:15 asubuhi ya Ijumaa, kwa mujibu wa NBC News.

No comments:
Post a Comment