Sunday, February 3, 2013

BOBBI KRISTINA AHUJUMU KITABU KINACHOELEZEA MAISHA YA WHITNEY HOUSTON...

Cissy Houston (kushoto) na Bobbi Kristina.
Bobbi Kristina, binti wa mwimbaji maarufu Whitney Houston, yuko kwenye mpango wa kuhakikisha kitabu cha bibi yake Cissy Houston kitakachoeleza kila kitu kinaanguka kwa kishindo na kuteketea ... kwa yeye pamoja na Nick kukisusia, na kuwaomba mashabiki wake kufanya kama hivyo.
Cissy alitoa kitabu wiki hii kinachoitwa "Kumbukumbu ya Whitney" ... ambacho kinasimulia kila kitu kuhusu maisha ya Whitney Houston ... na kufanya ziara mbalimbali kwenye vipindi vya televisheni kukifanyia promosheni.
Lakini Bobbi hakufurahishwa na hilo, akituma ujumbe katika mtandao wa Twitter kwa wafuatiliaji wake zaidi ya 119,000, "Chochote kuhusiana na kitabu cha bibi yangu, mimi na @nickgordon hakika siafikiniani naye."
Aliendelea, "Sijakisoma na sitakisoma ... Najiona nitakuwa nikimkosea heshima mama yangu na mimi kama binti yake sitakivumilia."
Cissy alikuwa kwenye kipindi cha Oprah wiki hii (akifanya promosheni ya kitabu hicho) na kukiri mahusiano yake na Bobbi Kristina yamezorota mno ... na kukiri alifahamu kwamba Bobbi alikuwa hataki kitabu hicho kiandikwe.

No comments: