Mtoto karudi nyumbani huku akilia njia nzima. Baba akamuuliza, "Unalia nini mwanangu?" Mtoto akajibu, "Mwalimu kanichapa viboko kumi!" Baba kwa hasira akamchukua mwanae hadi shuleni kukabiliana na mwalimu aliyemchapa mwanae. Alipofika akahoji sababu za mwanae kuchapwa na mwalimu akajibu, "Nimemuuliza Nairobi iko wapi, kashindwa kunijibu!" Baba akageuka na kumzaba kibao mwanae huku akifoka, "Nilishakukataza kuchezea vitu vya watu, sasa unaona! Haya Nairobi ya watu umepeleka wapi? Mie nitalipa na nini?" Duh, balaa...

No comments:
Post a Comment