![]() |
| Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani. |
Katibu Tawala wa Mkoa, Theresia Mmbando, alisema jana kuwa wanafunzi hao wataingia darasani baada ya vyumba vya madarasa 292 vinavyoendelea kujengwa na halmashauri za manispaa kukamilika.
Alisema kuwa katika madarasa hayo Ilala watajenga vyumba 70, Kinondoni vyumba 124 na Temeke madarasa 98. Pia alisema yatatengenezwa madawati 12,000.
“Wakurugenzi wa Manispaa zote tatu wameagizwa kuhamia katika shule au maeneo ambapo miundombinu hii inaendelea kujengwa ili kuhakikisha vyumba vyote vya madarasa vinakamilika kwa wakati.
“Tunataka wanafunzi hao wajiunge na shule hizo kama tulivyopanga na Sekretarieti ya Mkoa itafuatilia kwa karibu utekelezaji wa kazi hii,” alisema.
Alisema mwaka 2012 idadi ya wanafunzi 59,690 kati yao wavulana 28,569 na wasichana 31, 121, walisajiliwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi katika mkoa huo.
Hata hivyo, watahiniwa waliofanya mtihani huo ni 58,093 kati yao wavulana walikuwa 27,599 na wasichana 30, 494 ambao ni sawa na asilimia 97 ya waliosajiliwa.
Alisema kuwa wanafunzi waliofaulu mtihani huo ni 51,433 wakiwemo wavulana 24,506 na wasichana 26,927 sawa na asilimia 88.54 na kiwango cha ufaulu kwa mkoa huo kimepanda kwa asilimia 10 ikilinganishwa na mwaka 2011.
Alisema kuwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga katika shule mbalimbali za sekondari ni 39,681 kati yao wavulana 19,440 na wasichana 20, 241 sawa na asilimia 77 ambapo shule za ufaulu mzuri zaidi walikuwa wanafunzi 60, shule za ufundi wanafunzi 68 na shule za bweni kawaida wanafunzi 32.

No comments:
Post a Comment