Katika hali inayoonesha kuwa ni viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, Arusha, kuweweseka, sasa wameanza vitisho dhidi ya gazeti la HabariLeo huku wakitoa taarifa zisizojibu hoja za msingi za waumini wa kanisa hilo.
Wakati viongozi hao waliitisha mkutano wa waandishi wa habari wa vyombo vile wanavyodai ‘kuvimudu,’ baadhi ya waumini wameapa kuendelea na vita dhidi ya ufisadi ndani ya kanisa hilo hadi kieleweke.
Katika hali ya kushangaza, jana viongozi hao wakiongozwa na Ofisa Tawala wa Dayosisi hiyo, Emmanuel Saevie, waliwaita waandishi wa habari sita kutoa kile walichodai kuwa ni ufananuzi wa tuhuma mbalimbali zinazotolewa na waumini dhidi yao. HabariLeo halikualikwa.
Hata hivyo, taarifa hiyo iliyoitwa ya ufafanuzi haikuwa na majibu yoyote ya hoja za msingi zinazoendelea kutolewa dhidi ya viongozi hao na badala yake iliishia kutoa vitisho kwa HabariLeo na vyombo vingine vya habari vinavyofuatilia kwa karibu sakata hilo.
“Dayosisi inalitaka gazeti hilo kuomba radhi ndani ya siku saba, kinyume cha hapo, Dayosisi itachukua hatua kali za kisheria dhidi ya wahusika wote,” ilimalizia tishio hilo linalodaiwa kusainiwa na Askofu Thomas Laizer ambaye ni Mkuu wa Dayosisi hiyo la Januari 03, 2013.
Hata hivyo, habari kutoka kwa wasaidizi wa Askofu huyo zinasema kuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya rufaa ya Selian na wamekuwa na wasiwasi kama kweli anaweza kusaini tishio hilo kutokana na hali yake ya kiafya.
Taarifa hiyo (nakala tunayo), hata hivyo ina upungufu mwingi zaidi ya kuthibitisha kwa maandishi habari zilizokuwa zikitolewa na gazeti hili na kwenda mbali zaidi ya kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusiana na tuhuma hizo.
Tuhuma zilizothibitishwa kwa maandishi na taarifa hiyo ni pamoja na matatizo makubwa ya madeni yanayoikabili hoteli ya kitalii ya Arusha Corridor Springs, kusimamishwa na kufukuzwa kwa Meneja wa hoteli hiyo, John Njoroge Kiama na hata kufukuzwa uchungaji, Mchungaji Philemon Mollel wa Usharika wa Ngateu.
Uthibitisho mwingine wa habari zilizokuwa zinaandikwa na gazeti hilo kwa mujibu wa ‘ufafanuzi huo’ ni kuongezewa mkataba wa kazi kwa Katibu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Israel Karyongi hadi mwisho wa mwaka huu wakati umri wake wa kustaafu kwa mujibu wa Katiba ya Dayosisi hiyo, umepita.

No comments:
Post a Comment